mwanamke aishi na wanaume wawili kiunyumba miaka nane bila kutambuana.
MWANAMKE AISHI KINYUMBA NA WANAUME WAWILI KWA MIAKA NANE BILA KUTAMBUANA MBEYA Juliana Josia(22)kushoto anaedaiwa kuishi na wanaume wanaume wawili kwa zaidi ya miaka 8 bila kutambuana akiwa na Mume wake halisi Rogers ofisini kwa mtendaji Juliana Josia(22)kushoto akiwa na barozi Dinde Bwana Rogers akiongozana na baadhi ya viongozi wa mtaa kwenda kituo cha polisi Mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Juliana Josia(22)amezua utata hivi karibuni baada ya kugunduliwa akishi na wanaume wawili kwa muda wa miaka minane bila wanaume hao wawili kujitambua. Hayo yalibainika katika kituo cha Polisi Kati Jijini Mbeya baada ya Mwanamke huyo kudai kuporwa mtoto mgogoni jinsi ya kike mwenye umri wa miaka miwili eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya baada ya kutishiwa na Biton Bomani Mwashilindi mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya. Juliana alidai kuporwa mtoto na Biton Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi alipokuwa akielekea soko ...