Uchaguzi Kenya 2017: Mabalozi wataka wanaowania wakubali uamuzi wa wananchi
Image caption Katika baadhi ya maeneo Kenya, matembezi ya kuhimiza amani wakati wa uchaguzi yameandaliwa Mabalozi wa nchi za Magharibi wametoa wito kwa wagombea katika uchaguzi mkuu nchini Kenya kujiepusha na fujo na kuwahimiza wafuasi wao kutozua ghasia. Mabalozi hao wamesema viongozi wana wajibu wa kukataa ghasia na uchochezi. "Wagombea wanaposhindwa au washinde, wanafaa kuwa tayari kuukubali uamuzi wa wananchi kwa rehema na unyenyekevu," taarifa ya mabalozi hao imesema. Pande zote mbili zinafaa kuheshimu uhuru wa mahakama na ziwe tayari kutatua mizozo kuhusiana na uchaguzi kwa Amani "kupitia mahakama na si kuandamana kwa fujo barabarani." Chama cha Jubilee Jumatano kilikuwa kimemuomba Jaji Mkuu David Maraga amuondoe Jaji George Odunga kutoka kwenye majaji watakaosikiliza kesi kuhusu uchaguzi. Chama hicho kilikuwa kimesema Jaji Odunga ana uhusiano na baadhi ya viongozi wa muungano wa upinzani Nasa na hawezi kutarajiwa atoe uamuzi wa haki bila kuegeme...