Posts

Showing posts from July 24, 2017

LORI LAPINDUKA DARAJA MTO SONGWE NA KUZIBA BARABARA

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipenya ili kuvuka katika daraja la mto Songwe kwenye mpaka wa mikoa ya Mbeya na Songwa baada ya Lori lililokuwa limebeba vinywaji baridi kupinduka katika daraja hilo na kuziba barabara. Ajali hiyo ilisababisha msururu mrefu wa magari yaliyokuwa yakitoka Tunduma na yale yaliyokuwa yakitoka Mbeya Julai 24, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Msururu wa magari uliosababishwa na ajali ya lori lililopinduka kwenye daraja la mto Songwe katika barabara Mbeya- Tunduma Julai 24, 2017. Lori hilo lilikuwa limebeba vinywaji baridi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UKWELI KUHUSU MZEE MAJUTO, NA TETESI ZA KUFA

Image
MSANII wa filamu nchini,  Haji Salum maarufu kama Mboto , amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni  zinazodai kuwa nguli wa  vichekesho  katika tasnia ya  uigizaji , Amri Athuman maarufu kama  King Majuto  amefariki dunia. Mboto baada ya kupata taarifa hizi alifunga safari kuelekea  mkoani  Tanga  ambapo ni nyumbani kwa Mzee Majuto  na kumkuta hai, na amekanusha uvumi huo kupitia ukurasa wake wa  Instagram  kwa kuposti picha inayowaonyesha yeye na  Majuto  wakiwa nyumbani kwake, na picha hiyo iliambatana na maneno yafuatayo: “ Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu  Mzee Majuto  nimelazimika kuja kwake  Tanga . Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizuri na si kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunaye. Kwa sasa mzee ni mzima nipo naye  Tanga ,” ameandika  Mboto . Siku chache zilizopita,  gazeti la Ijumaa  Wikienda liliripoti taarifa za kuumwa kwa  Mzee Majuto...

Shetta: Mimi ni Chawa Kwa Matajiri Siwezi Kufa Njaa.

Image
Msanii Shetta ametaka watu wasimuhisi kuwa anajishughulisha na biashara za madawa na badala yake watambue yeye ni mtu anayetumia fursa kila aonapo na ndio maana ana marafiki wengi matajiri ambao wanamsaidia. Akizungumza kwenye Planet Bongo East Africa radio, Shetta amesema kwamba yeye hajishughulishi na biashara hizo za madawa na wala hana pesa za kutisha kama jinsi watu wanavyomfikiria. "Mimi sina fedha nyingi kama watu wanavyodhani, sema nina fedha za kutosheleza maisha yangu. Ningekuwa nina pesa nisingwekuwa nawaganda matajiri. Mimi ni chawa kwa matajiri nikiwa nashida namcheki boss Mo, au matajiri ambao nimetengeneza ukaribu nao na mwisho wa siku mambo yangu yanaenda," Shetta. Katika hatua nyingine Sheta amesema yeye ni mtu ambaye anapenda vitu vizuri na ndiyo sababu watu wengi wamekuwa wakimfikiria vibaya 'Ningekuwa nauza madawa ningekuwa na mimi kwenye ile orodha iliyowahi kupelekwa pale polisi. Mimi ni mtu ambaye napenda vitu vizuri na nikikitak...