NAIBU SPIKA AFUNGUA MASHIDANO YA MBIO ZA BAISKELI MKOANI SIMIYU
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (wa pili kushoto) akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi (kulia) ni Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products ambayo ni mdhamini, Mhe.Salum Khamis akimpongeza Mshindi huyo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye bendera nyeupe kulia) akifungua mashindano ya Mbio za Baiskeli Mkoa wa Simiyu(Simiyu Jambo Festival) kwa kuruhusu washiri kuanza mashindano hayo Mjini Bariadi. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye baiskeli wa pili kulia) akiwa na viongozi wa Mkoa na baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Simiyu na Viti Maalum kutoka nje ya Mkoa kwa ajili ya kufungua mashindano ya baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi. Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products, Mhe.Salum Hamis ambaye ndio mdhamini wa mashindano ya baiskeli n...