Posts

Showing posts from October 20, 2017

MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE OKTOBA 20, 2017

Image

Msimamo wa Acacia kuhusu makubaliano ya Barrick na Serikali

Image
Kampuni ya uchimbaji madini nchini Tanzania, Acacia imesema kuwa inafahamu kuhusu serikali ya Tanzania na Barrick Gold Corporation (“Barrick”), kuwa wamefanya mkutano kwa ajili ya kushirikishana makubaliano yaliyofikiwa kutoka kwenye mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu Oktoba 19 kati ya serikali ya Tanzania na Barrick ambaye ndiye mwenye hisa kuwa (asilimia 64) katika Kampuni ya Acacia. Katika taarifa yake iliyoitoa jana kwenye tovuti yao, Acacia wameeleza kuwa wamepata nakala ya makubaliano hayo, na kwa sasa wanatafuta ufafanuzi zaidi. Acacia wameeleza kuwa hawakupewa taarifa yoyote rasmi kuhusu makubaliano hayo yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili na wao waweze kuyafikiria. Wameeleza kwamba, kama ambavyo walisema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa, makubaliano yoyote yatakayofikiwa kati ya serikali na Barrick, ni lazima yaridhiwe na Acacia. Aidha, wamesema watafikiria kuhusu makubaliano hayo mara watakapopata taarifa za...

Wema Sepetu Ataja Sababu Zilizomfanya Asiende Kumuona Tundu Lissu

Image
Mrembo wa Tanzania na Kada wa Chadema Wema Sepetu ametoa ya Moyoni kwa nini hakwenda kumuona mapema Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi septemba 7  ni kwamba asingeweza kumuona akiwa kwenye maumivu. Wema ameweka wazi maneno hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni baada ya dakika chache tangu kuachiwa kwa picha za kwanza za Mbunge huyo akiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya. Wema ameandika "Kisichokuua kinakufanya uwe na nguvuz zaidi....Utarudi tena ukiwa na nguvu kuliko ulivyokuwa awali...Shujaa wetu. ... Picha hii imenifanya nipate hisia. Sasa naweza andaa safari ya Nairobi kuja kukuona.. Awali nisingeweza kuvumilia kukuona ukiwa kwenye maumivu".  Wema Sepetu ametajwa na Chama cha  Chadema kama mmoja wa wahamasishaji  aliyeweza kuhamasisha watu kutoa michango kwa ajili ya matibabu ya Mbunge Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa kwenye gari lake nje ya ma...

Waingereza watupwa nje Luxembourg Open

Image
Image caption Heather anashikilia nafasi ya 85 duniani Wacheza tennis waingereza Heather Watson na Naomi Brady kwa pamoja wametupwa nje ya michuano ya Luxembourg Open katika hatua ya robo fainali. Watson namba mbili kwa ubora nchini Uingereza namba 81 duniani amepoteza kwa seti 6-4 6-4 mbele ya Elise Mertens wa Ubelgiji. Kwa upande wa Naomi Broady amechapwa na Monica Puig wa Puerto Rico kwa seti 6-0 5-7 6-1. Puig atakutana na Elise Mertens katika hatua ya nusu fainali na Pauline Parmentier wa Ufaransa atacheza na Caroline Witthoft wa Ujerumani.

Wakuu wa zamani wa riadha wakamatwa kwa rushwa

Image
Image caption Papa Massata amesema tuhuma hizo ni sawa na fitina Mkuu wa zamani wa wa shirikisho la riadha ulimwenguni Lamine Diack na mwanae Papa Massata wamekamatwa nchini Brazil kwa tuhuma za rushwa. Tiyari wanashutumiwa kwa tuhuma kama hizo nchini Ufaransa kwa kupokea dola milioni 2 kwa ajili ya kuufanya mji wa Rio kuwa muandaaji wa michuano ya Olimpiki mwaka uliopita. Image caption Lamine Diack ameongoza shirikisho la riadha tokea mwaka 1999 mpaka 2015 Lamin kwa sasa anashikiliwa nchini Ufaransa na tiyari amenyanganywa hati yake ya kusafiria huku Papa Massata akiwa amejificha nchini kwao Senegal. Awali wawili hao walikana mashitaka ya kuhusika katika rushwa hiyo.

Arsenal yapata ushindi wa tatu mfululizo Yuropa

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud akisheherekea bao lake Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa kikosi chake kilionyesha ujasiri huku kikiendeleza mwanzo mzuri wa kuwania kombe la Yuropa baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya Crvena Zvezda huko Serbia. Bao zuri la Olivier Giroud's katika dakika za lala salama ziliipatia Arsenal ushindi wa tatu mfululizo katika kombe hilo na hivyobasi kupnda hadi kilele cha kundi H wakiwa na alama tano juu ya BATE Borisov. ''Nadhani tuna ari ya kushinda '', alisema Wenger. ''hatukulaza damu nabtulitaka kupata nbao kila mara''. Ujasiri wa wachezaji wa Arsenal ulijadiliwa wakati waliposhindwa 2-1 na Watford siku ya Jumamosi , huku mshambuliaji Troy Deeney akisema kuwa The Gunners hawana motisha. Wenger alikiri kabla ya mechi hiyo kwamba matamshi hayo yalimuudhi , lakini akasema kuwa wachezaji wake watajibu kwa kuonyesha mchezo mzuri huk...

Xavi: Neymar alitaka kujiunga na PSG katika harusi ya Messi

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Neymar baada ya kujiunga na PSG Nahodha wa zamani wa Barcelona Xavi amefichua kuwa Neymar alifichua habari za kutaka kujiunga na klabu ya PSG katika harusi ya Lionel Messi. Ripoti za Neymar kutaka kuondoka Barcelona msimu uliopita na kuhusishwa kwake na PSG zilianza kubainika lakini zikashika kas,i na kufikia Agosti 3 Neymar alijiunga na PSG hadi 2022 kwa kitita kilichovunja rekodi ya dunia cha £198m. Lakini kulingana na Xavi, Neymar alifichua mpango huo mwezi mmoja kabla katika harusi ya Lionel Messi wakati mshindi huyo wa mataji 5 ya mchezaji bora Ballon d'Or alipofunga ndoa na mpenziwe wa miaka mingi Antonella Roccuzzo nchini Argentina. Raia huyo wa Brazil aliwaambia rafikize kuhusu azma yake ya kutaka kuondoka. Akizungumza na BBC , Xavi ambaye aliichezea Barcelona mechi 700 na kushinda mataji 8 ya La Liga pamoja na makombe manne ya vilabu bingwa Ulaya alisema. Alituambia siku ya harusi ya Messi kwamba anataka maba...

Obama na Bush wakosoa uongozi wa Trump

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES/REUTERS Image caption Marais wa zamani Barrack Obama na George Bush Marais wawili wa zamani nchini Marekani wameonyesha wasiwasi wao kuhusu hali ya kisiasa nchini humo bila kumtaja rais Donald Trump kwa jina. Barrack Obama aliwataka wapiga kura kukataa kile alichokitaja kuwa siasa za kuwagawanya watu mbali na siasa za hofu. Alikuwa akimfanyia kampeni mgombea wa chama cha Democrat anayewania wadhfa wa gavana wa jimbo la New Jersey. Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya mtangulizi wake George W. Bush kukosoa unyanyasaji na chuki katika maisha ya kawaida ya raia Marekani. Katika hotuba, alisema chuki dhidi ya wale wanaokupinga zimeongezwa nguvu huku maadili ya kiraia yakisahaulika. Bwana Trump ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa mtangulizi wake bado hajatoa tamko lolote. Marais wa zamani nchini Marekani kwa kawaida huwa nadra kutoa maoni yao kuhusu hali ya kisiasa na ilionekana kuwa makosa makubwa kwa rais aliyetangulia kumkosoa mrith...

Korea Kaskazini yaionya Australia kutoshirikiana na Marekani

Image
Haki miliki ya picha KOREAN CENTRAL NEWS AGENCY Image caption Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un Serikali ya Australia imesema kuwa imepokea stakhabadhi kutoka Korea Kaskazini ikiitaka Canbera kutojihusisha na utawala wa rais Trump. Barua hiyo imeshutumu onyo la Marekani kwamba itaiangamiza Korea Kaskazini iwapo italazimika kujilinda. Waziri mkuu wa Australia PM Malcolm Turnbull amesema kuwa barua hiyo pia ilimwa kwa mataifa mengine. Amesema inaonyesha kuwa shinikizo za kidiplomasia dhidi ya Korea Kaskzini zimeanza kufanya kazi, licha ya barua hiyo kuwa na ufyozi na malalamishi ya kawaida ya taifa hilo. Barua hiyo yenye ukurasa mmoja ilitumwa kupitia ubalozi wa Korea Kaskazini nchini Indonesia na inadaiwa kutoka kwa kamati ya maswala ya kigeni ya Korea Kaskazini. Imezitaka serikali nyengine kujitenga na hatua zisizokuwa na heshima za rais Trump ikisisitiza kuwa Marekani inaweza kusababisha janga kubwa la kinyuklia. Bwana Turnbull amesema kuwa Korea Kaskazini ndio ina...