Chama cha mawakili Kenya chamkosoa Uhuru Kenyatta
Haki miliki ya picha FACEBOOKK Image caption Rais wa LSK Isaac Okero Chama cha mawakili nchini Kenya LSK kimemkosoa rais Uhuru Kenyatta wa Kenya dhidi ya kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu kufuatia uamuzi wa kubatilisha uchaguzi wake. Rais wa LSK Isaac Okero katika taarifa siku ya Jumamosi alimkosoa rais Kenyatta kwa kumtaja jaji mkuu David Maraga na majaji wengine wa mahakama hiyo kuwa ''wakora''. Rais Kenyatta alitoa matamshi hayo wakati wa ziara ya kukutana na wafuasi wake katika soko la Burma mjini Nairobi siku ya Ijumaa muda mfupi baada ya mahakama hiyo ikiongozwa na jaji Maraga kufutilia mbali uchaguzi wake. Bwana Okero alisema: Matamshi ya rais kwamba majaji hao wasubiri rais Uhuru Kenyatta achaguliwe katika uchaguzi ujao hayafai kutoka kwa kiongozi wa taifa ambaye chini ya katiba ya Kenya ni nembo ya umoja wa Wakenya. Amesema kuwa rais Kenyatta anapaswa kulinda haki ya majaji na idara yote ya mahakama. Bwana Okero amesema kuwa ijapokuwa rais...