Posts

Showing posts from October 18, 2017

Rais Kenyatta aitisha maombi kabla ya marudio ya Uchaguzi

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Rais Kenyatta aitisha maombi kabla ya marudio ya Uchaguzi Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa nchi itafanya maombi mwisho wa wiki hii kabla ya marudio ya uchaguzi mkuu wa wiki ijayo. Taarifa ya Rais Kenyatta ilikuja baada ya afisa wa cheo ya juu kwenye tume ya uchaguzi nchini Kenya, kukimbia nchi akisema kuwa amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa. Roselyne Akombe aliiambia BBC kuwa marudio ya uchaguzi, hayaafikii matarajio ya uchaguzi ulio huru na wa haki. Bw. Kenyatta alisema kuwa wakenya watatumia wikendi kwa maombi na maridhiano kabla ya marudio ya uchaguzi wa urais ambao utafanyika tarehe 26 mwezi Oktoba. Mpinzani wake mkuu Raila Odinga alijiondoa kutoka kwa uchaguzi huo wiki iliyopita. Hata hivyo Rais Kenyatta hakuzungumzia kujiuzulu kwa Bi Akombe.

Raila Odinga aitisha maandamano ya nchi nzima siku ya uchaguzi Kenya

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Raila Odinga aitisha maandamano siku ya uchaguzi Kenya Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya (Nasa), Raila Odinga, amesema kuwa upinzani utafanya maandamano ya nchi nzima tarehe 26 Okotoba. Hii ndiyo siku ya kufanyika marudio ya uchaguzi wa urais. Akihutubia wafuasi wake katika mtaa wa Kamukunji mjini Nairobi leo Jumatano, Bw. Odinga alisema kuwa ataendelea kushikiza Marekebisho katika tume ya uchaguzi ili kuweza kufanyinya uchaguzi ulio wa haki. "Leo tunabadilisha kauli mbiu yetu kutoka "hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi" hadi "hakuna uchaguzi Oktoba," Bw. Odinga alisema huku akisisitiza kuwa amejiondoa kutoka kwa uchaguzi huo. Bw. Odinga alitoa tangazo hilo hata baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuonya kuwa hatua kali zinachukuliwa dhidi ya yeyote ambaye atajaribu kuvuruga marudio ya uchaguzi. Akizungumza eneo la Nanyuki, Rais Kenyatta alilaani visa ambapo maafisa wa IEBC walishambuliwa wakati waki...