Posts

Showing posts from August 22, 2017

PICHA 13: Rais wa Zanzibar alivyozindua Madarasa katika Skuli ya Msingi Kijitoupele.

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein August 21, 2017 aliweka Jiwe la Msingi kuzindua madarasa matatu yaliyojengwa kwa Siku 11 chini ya Kampeni ya ‘Mimi na Wewe’ inayosimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghalibi Ayub Mohammed Mahmoud.

Trump aapa kuwa atashinda vita Afghanistan

Image
Image caption Trump amesema ataongeza idadi ya wanajeshi Afghanistan Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka nchini Afghanistan kutaacha pengo ambalo huenda likajazwa na magaidi. Alisema kuwa mapango yake ilikuwa ni ya kuondoa vikosi vya Marekani, lakini badala yake ameamua wanajeshi hao kubakia ili kuzuia kurudia makosa ambao yalitokea nchini Iraq. Amesema pia kuwa anaongeza idadi ya wanajeshi watakao pelekwa nchini Afghanstan. Akizungumza kupitia Televishen, Rais Trump amesisitiza kuwa kipaumbele cha Marekani ni kutekeleza masuala yenye maslahi katika usalama wa taifa hilo, kutokomeza mtandao wa ugaidi. Image caption Trump amesema ni vigumu kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini humo Amesisitiza pia kuwa kitendo cha Marekani kujiondoa kwa haraka Afghanistan, kitatatoa mwanya kwa ugaidi kujiimarisha zaidi kama ilivyotokea Iraq. Hata hivyo Trump amekwepa kuzungumzia moja kwa moja muda wa mwisho wa ushiriki wa Marekani nc...

Wanaume 4 washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini

Image
Sambaza habari hii Messenge Image caption Wanaume 4 washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini Wanaume wanne wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu. Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu. Kisha polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilipatikana. Wanaume wanne, wawili kati yao madaktari wa kitamaduni walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua. Walifikishwa katika mahakama ya Estcourt kilomita 175 kaskazini magharibi mwa mji wa Durban. Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa kuna uwezekano kuwa wanaume hao wanne walio na umri wa kati ya miaka 22 na 32 ni sehemu ya genge kubwa. Uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa zao wametowew...

Jenerali wa Jeshi Ateuliwa na Rais Magufuli Kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

Image
Raisi John Magufuli leo August 21, 2017 amemteua Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Uteuzi wa Brigedia Jenerali John Julius Mbungo unaanza leo August 21, 2017.

Mjenga misuli ala kondo la nyuma la mpenziwe

Mjenga misuli ala kondo la nyuma la mpenziwe Sambaza habari hii Email   Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya pichaAP Image caption Wajenga misuli, Australia Mjenga misuli ambaye alipata umaarufu kwenye mtandao baada ya kuchoma na kula kondo la nyuma la mpenzi wake amesema kondo hiyo lililokuwa kama maini.  Mwamume huyo mwenye umri wa miaka 32 kutoka Australia amesema atakuwa 'makini' jinsi kondo hiyo ingeonja. ''Mpenzi wangu hakuwa na shida nami kula nyama hiyo, lakini nilipoianza kuichoma jikoni, sidhani alipenda, Aaron Curtis amesema. ''Haikuwa na ladha tofauti lakini ngozi yake ilinikumbusha maini.''  Coleen Rooney kula kondo la nyuma Wakati wa uja uzito, kondo la nyuma husambaza chakula kutoka kwa mama hadi kwa mtoto. Kwa mzazi kula kondo hiyo, baada ya kujifungua, si jambo la kushangaza kwamba kondo hiyo ina virutubisho vya kiasili. Nimekuwa na maoni tofauti kuhusiana na kutupa chakula, kwa hivyo ulaji wa kondo hiyo halikuwa jambo kubwa kwake ,...