Posts

Showing posts from December 3, 2017

Trump kutambua Jerusalem ni mji mkuu wa Israel

Image
Image caption Donald Trump kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel Maafisa nchini Marekani wanasema kuwa Rais Trump anatarajiwa kutangaza wiki ijayo kuwa Marekani inatambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel hatua ambayo wakosoaji wanasema kuwa itachochea mzozo zaidi katika eneo hilo. Hali kamili ya mji huo inakumbwa na utata huku pande zote mbili za Israel na Palestina zikidai kuwa ndio mji wao mkuu. Trump alitoa ahadi ya kampeni ya kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem. Image caption Mji wa Jerusalem Mwandishi wa BBC anasema kwa kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, Trump anaashiria hatua ya kutekeleza ahadi yake ya kampeni.

Hawaii yafanyia jaribio king'ora cha kuonya shambulizi la nyuklia

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Hawaii yafanyia jaribio king'ora cha kuonya kuhusu shambulizi la nyuklia Kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa vita baridi jimbo la Hawaii nchini Marekani limefanyia jaribio king'ora cha kuonya kuhusu shambulizi la nyuklia Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya jaribio la kombora la masafa marefu lililofanywa na Korea Kaskazini mapema wiki hii. Hawai kawaida ina ving'ora ambavyo huonya kuhusu majanga ya asili kama tsunami. Kingora cha nyuklia kina mlio tofauti ambacho huwaonya watu kusalia manyumbani wakisubiri ushauri zaidi. Lakini king'ora hicho kilisikika tena Ijumaa na kitarudiwa klila jumatatu ya kwanza ya mwezi. Kombora linalorushwa kutoka Korea Kaskazini linaweza kushambulia Hawaii ndani ya dakika 20 baada ya kufyatuliwa. Hivi majuzi Korea ilifyatua kombora mpya la masafa marefu ambalo inadai kuwa linaweza kushambulia ndani ya Marekani. Image caption Kombora linalorushwa kutoka Korea Kaskazini linaweza k...

Trump adaiwa kumtetea Michael Flynn dhidi ya FBI

Image
Image caption Trump adaiwa kumtetea Michael Flynn dhidi ya FBI Rais Donald Trump amezua shutuma kwamba huenda alizuia haki kutendeka baada ya kutuma ujumbe katika mtandao wa Twitter kwamba alimfuta kazi mshauri wake wa maswala ya usalama Michael Flynn kwa sababu aliwadanganya maafisa wa FBI. Baadhi ya wataalam wa maswala ya sheria wanasema kuwa matamshi yake yalionyesha kuwa bwana Trump alijua kwamba mshauri wake wa zamani alikuwa amewahadaa wachunguzi wakati alipomtaka mkurugenzi wa zamani wa FBI James Comey kusitisha uchunguzi dhidi yake. Rais huyo alisisitiza kuwa vitendo vya mshauri wake wa zamani vilifuata sheria.  Siku ya ijumaa Michael Flynn alikuwa mwanachama wa kwanza wa utawala wa rais Trump kushtakiwa kufuatia uchunguzi kuhusu hatua ya Urusi kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka jana. Wakati huohuo Chombo cha habari cha Marekani ABC, kimemsimamisha kazi kwa muda mwandishi wake wa maswala ya uchunguzi , Brian Ross kufuatia makosa katika ripoti yake k...

Mange Kimambi Aibua Mapya Wema Kurudi CCM

Image
Mwanadada Mange Kimambi ameibukia sakata la Wema Sepetu kurudi CCM,ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu atabiri mpango wa Wema Kurudi CCM. Akizungumza kupitia  ukurasa wake wa mitandao ya kijamii Kimambi amesema Wema  hajawaangusha watanzania  pekee bali  amejiangusha yeye  mwenyewe kwa kutokua na msimamo. “Hujawaangusha waTZ tu, umejiangusha mwenyewe pia, your fans and everyone who cared for you. Hivi kizazi hiki kina Winnie Mandela hakuna kabisa eehe? Nakuonea huruma mnoooo sababu umepoteza credibly yooooote kwenye jamii” Ameandikia Mange Kimambi. Hivi karibuni Mange alisema kuwa anazo taarifa za uhakika kuwa Wema Sepetu pamoja na Mama yake watarudi chama cha Mapinduzi akidai kuwa mama yake amekubali kurudi isipokuwa anasuburiwa yeye. Mange alisema mpango wa kurudi CCM unafuatia Wema na Mama yake kubanwa katika mambo  mbalimbali kutokana na kuwa upande wa upinzani. Wakati akitangaza kurudi CCM jana Wema alisema.. “Siwezi Kuendel...