SIMBA VS YANGA NANI KULIA NANI KUCHEKA?, HII NI MECHI YA 'UTATOA HUTOI' TUKUTANE KESHO TAIFA
*Huku Ajib, Tshishimbi na Ngoma *Kule Okwi, Niyonzima na Gyan *Matokeo yatadhihirisha usajili wa vikosi bora kati ya Lwandamina na Omog MATOKEO YA MECHI ZA NGAO YA JAMII 2008- Yanga 2-Simba 1 2009- Mtibwa Sugar 1- Yanga 0 2010- Yanga 0- Simba -ikapigwa mikwaju ya penati, Yanga 3-Simba 1 2001- Simba 2- Yanga 0 2012- Simba 3- Azam 2 2013- Yanga 1- Azam 0 2014- Yanga 3- Azam 0 2015- Yanga 2- Azam 2 ikapigwa mikwaju ya penati, Yanga 8- Azam 7 2016- Azam 4- Yanga 1 2017- Yanga ?- Simba ? Na Abdul Dunia, Dar KUMBUKUMBU zinanirudisha miaka mitatu nyuma. Kilinukishwa pale Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Ilikuwa bonge la mechi kali isiyo na mfanowe. Katika dakika 90 za mtanange huo yalishuhudiwa mabao sita. Hakika ilikuwa mechi ya haja. Yalitokea matukio kibao katika mtanange huo ikiwa ni pamoja na baadhi ya mashabiki kuzimia. Wachezaji walitaharuki, maaskari na matabibu wa huduma ya kwanza wote walikuwa bize siku h...