Posts

Showing posts from August 26, 2017

Video ya dakika 2 ikionyesha Hat-Trick ya Okwi iliyookoa Milioni 5

Image

Hizi Ndizo Mbinu Bora Za Kuepuka Majanga Kwenye Uwekezaji Wako Wa Majengo.

Image
Wakati tulionao sasa ni wakati bora sana wa sisi kuendelea kupeana hamasa katika kuzitumia rasilimali zetu katika kujiletea maendeleo yetu binafsi pamoja na nchi yetu kwa ujumla. Hatuna sababu zozote za kukata tamaa pale mambo yanapokuwa magumu na hakuna dalili yoyote ya wewe kusonga mbele, bali kwetu inapaswa kuwa fursa ya kutafakari upya na kuchukua hatua bora zaidi zitakazotusaidia kutimiza malengo yetu. Nidhamu na juhudi ndiyo nguzo yetu katika kufanikisha kila jambo ambalo tumeamua kulifanyia kazi. Pamoja na hayo zipo changamoto za kimazingira katika uwekezaji wa majengo ambazo zinatokana na usimamizi na mabadiliko ya kisera na kisheria ambazo si za mtu mmoja bali ni za nchi kwa ujumla. Kiini cha mabadiliko hayo ni maendeleo ya kiuchumi na uboreshaji wa mazingira katika kuifanya nchi yetu kuwa mahali bora na salama kwa kila mmoja wetu.  Mabadiliko haya yanawaathiri baadhi ya marafiki zetu ambao wamejikuta wakiguswa kwa namna tofauti. Njia pekee katika kutatua ch...

Tanzania yakataa wakimbizi wa Burundi nchini humo

Image
Image caption Wakimbizi wa Burundi walioingia Tanzania Serikali ya Tanzania imelipatia shirika la wakimbizi duniani UNHCR siku saba kuanza kuwarudisha wakimbizi wa Burundi ambao wanataka kurudi kwao kwa hiari, ama sivyo serikali yenyewe itafanya zoezi hilo yenyewe. Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Mwigulu Nchemba ametoa agizo hilo siku ya Alhamisi alipokuwa katika ziara ya kikazi katika kambi ya Nduta Magharibi mwa Tanzania ambayo ni moja ya kambi zinazohifadhi wakimbizi wengi wa Burundi. Tanzania ndio nchi inayoongoza Afrika Mashariki kwa kuhifadhi wakimbizi wengi kutoka Burundi. Bwana Nchemba amewashutumu maafisa wa UNHCR kwa kuchelewesha zoezi hilo la kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa Burundi wanaotaka kurejea nchini kwao kwa hiari. Enable it in your browser or pata Flash Player hapa. Samahani, unahitaji Flash kucheza taarifa hii Tanzania yatahadharisha wahalifu waliotoka Burundi Zaidi ya wakimbizi elfu 8 kati ya laki moja ishirini...