Posts

Showing posts from November 17, 2017

Polisi walivyokamata watu leo Kariakoo… mtaa kwa mtaa

Image
Ni Habari kutoka Kariakoo Dar es salaam ambako watu mbalimbali wamekamatwa na Polisi baada ya kukutwa na makosa ambayo yalishatangazwa hapo awali kupitia vyombo vya habari. Mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa kushirikiana na Wakala wao kampuni ya Msama Auction Mart wanaendelea na ukaguzi maalum mtaa kwa mtaa Dar es Salaam kukagua na kuhakikisha CD zote zinazouzwa zina sticker ya TRA ili kukusanya mapato. Leo November 16 kwa kushitukiza ukaguzi umepita duka kwa duka ukiongozwa na Mkurugenzi wa Msama Auction Mart Alex Msama na kukamata wanaoingiza nyimbo kwenye simu, CD zisizokuwa na stika na waliokutwa wote wamekiuka masharti hayo hivyo wamechuliwa Polisi, tazama hii video hapa chini kuona ilivyokua Polisi walivyokamata watu Kariakoo

Emmerson Mnangagwa: 'Mamba' ambaye amegeuka kumuuma Mugabe

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Mnangagwa amekuwa miongoni mwa waliotarajiwa kumrithi Mugabe Imekuwa siri ya wazi nchini Zimbabwe kwa miaka mingi kuwa Emmerson Mnangagwa angechukua nafasi ya Robert Mugabe na kuwa rais. Lakini Bwana Mugabe alionekana kucheza na hisia zake- wakati mwingine akimpandisha cheo ndani ya chama tawala cha Zanu- PF na serikalini na kuongeza tetesi ya yeye kuwa mrithi mtarajiwa lakini baadaye alishushwa cheo baada ya Mnangagwa kuonekana kuonesha nia zake mapema mno. Baada ya kutenguliwa, imeonekana kama subira ya mwanaume huyo maarufu kama "mamba" hatimaye imeisha. Baada ya Rais Mugabe kumtengua na kumshutumu kwa mfisadi, wafuasi wake na vikosi vya usalama waliingilia kati kwa niaba yake. Haki miliki ya picha AFP Image caption Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe Constantino Chiwenga (kushoto) ni rafiki wa karibu wa Mnangagwa Mnangagwa alisaidia kuongoza vita vya kupigania uhuru vya Zimbabwe na baadaye kuwa jasusi mkuu wa nchi wakati wa mg...

Mkuu wa zamani wa soka Amerika Kusini kushitakiwa kwa rushwa

Image
Image caption Nicolás Leoz ameliongoza shirikisho la soka Amerika ya Kusini kwa miaka 27 Jaji mmoja nchini Paraguay ameruhusu upelelezi kuanza kwa mkuu wa zamani wa shirikisho la soka la Amerika ya Kusini Nicolas Leoz kwa tuhuma za rushwa. Leoz ni mmoja ya watuhumiwa wakubwa wa rushwa waliotajwa na mahakama moja nchini Marekani. Bosi huyo wa zamani wa FIFA amekuwa chini ya uangalizi mkali nyumbani kwake Asuncion Paraguay. Anatuhumiwa pia kupokea rushwa ili kuiruhusu Qatar kuandaa kombe la dunia mwaka 2022. Leoz anasema tuhuma hizo ni za uongo huku mwanasheria wake akiapa kukata rufaa.

Nadal kulipwa $14000 kama fidia ya kuharibiwa jina

Image
Image caption Rafael Nadal anashikilia namba moja kwa ubora duniani Mahakama mjini Paris imemuamuru waziri wa michezo wa Ufaransa Roselyne Bachelot kumlipa mcheza tennis nyota Rafael Nadal kiasi cha dola za kimarekani 14,000 kutokana na kumtuhumu kutumia dawa zilizokataliwa michezoni. Nadal alimfungulia mashitaka kwa kauli yake hiyo kwa kusema imemuharibia taswira yake kwa jamii. Awali Nadal alitaka dola laki moja lakini kutokana na ushauri wa watu akaamua kupunguza. Mchezaji huyo namba moja duniani amesema fedha hizo atazitumia kusaidia wasiojiweza nchini Ufaransa.

Kampuni ya Uswisi yafungua kiwanda cha kemikali Tanzania

Image
Image caption Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli Kampuni kutoka nchini Uswisi imefungua kiwanda cha kemikali za ujenzi na zile zinazotumika katika magari. Florence Tinguely Mattli ni balozi wa Uswisi nchini Tanzania, ameiambia BBC kuwa suala la uwekezaji ni hatua ya kujiamini kwanza na kutoona hasara. Alipoulizwa kuhusiana na sera za uwekezaji nchini Tanzania kudaiwa kuwa si rafiki Bi.Mattli amesisitiza kuwa uzoefu wao kiviwanda na kuwekeza katika mataifa mbalimbali duniani itawasaidia kujua ni mambo gani ya kuzingatiwa katika uwekezaji wao Tanzania katika serikali ya awamu ya sasa. Image caption Kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya elfu moja Waziri wa viwanda wa Tanzania Dr Charles Mwijage anasema kuwa dira ya mwaka 2025 ni kuhusiana na viwanja. Meneja mkuu wa kiwanda hiki cha Kemikali cha Sika Tanzania Alfonso Paradinas anasema kiwanda chake kitazalisha kemikali hizo za ujenzi na kuongeza ubora wa majengo nchini humo. Hata hivy...

Mugabe 'akataa wito wa kumtaka ajiuzulu'

Image
Haki miliki ya picha AFP / ZBC  Image caption Mugabe (wa pili kulia) akiwa kuzuizi cha nyumbani akisimama na mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga (kulia) Rais wa miaka mingi nchini Zimbabwe anaripotiwa kukataa kuandoka madarakana mara moja licha ya kuongezeka wito wa kumtaka ajiuzulu. Mugabe, 93 aliwekwa chini ya kuzuizi cha nyumbani wakati jieshi lilichukua madaraka siku ya Jumatano kufuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi. Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mazungumzo yaliyofanywa Muganbe na ujumbe kutoka kanda hiyo pamoja na mapema. Lakini taarifa zinasema kuwa amekataa kuondoka madarakani. Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai alisema mapema kuwa kwa manufaa ya watu Mugabe anastahili kujiuzulu mara moja. Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Robert Mugabe alikutana na mkuu wa majeshi aliyeongoza hatua dhidi yake Jeshi lilichukua hatua baada ya Rais Mugabe kumfuta makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa, wiki iliyopiya, na kuashiria kuwa alimpendelea mke...

WANANCHI WA BOLISA KUPATA SHULE MPYA YA SEKONDARI

Image
Wananchi wa kata ya Bolisa wanatarajia kujengewa shule mpya ya sekondari ya kata ili kuondokana na  tatizo la umbali kwa wanafunzi  wa kata hiyo, amebainisha na Mkurugenzi wa Mji Kondoa Bw. Khalifa Kondo alipokuwa akijibu swali wakati wa mkutano wa wananchi  wa kata ya Bolisa na Mkuu wa Mkoa  alipofanya ziara ya kujitambulisha wilayani humo hivi karibuni.   "Shule ya Gubali imeshughulikiwa na wananchi wa kata ya Gulisa kabla ya kugawanywa kuwa kata mbili lakini kwasasa kata ipo kata ya Kolo tunaomba kujua mipaka ya kata hizi mbili ili shule ya Gubali ibaki Bolisa".aliuliza bwana Abubakari Mussa. Akifafanua Bwana Kondo alisema kuwa ni kweli shule hiyo ipo lakini kutokana na mazingira ya shule hiyo wameanza kupata fedha za kujenga mabweni  katika shule ya  Sekondari Gubali  kwa ajili ya wanafunzi  kutoka nchi nzima na si Kolo tu.  Kondo aliendelea kufafanua kuwa kutokana na mipango hiyo wilaya imejipanga k...