Posts

Showing posts from December 15, 2017

Polisi India wafunga akaunti ya mtuhumiwa wa mauaji

Image
Image caption Shambhu Lal katika picha inayomuonyesha akimnyanyasa mtu huyo Polisi katika jimbo la Rajasthan nchini India wamefunga akaunti ya benki ya mtu anayehusishwa na mauaji ya muislamu mmoja. Inasema zaidi ya dola elfu nne zilishachangiwa kwenye akaunti yake kabla ya kufungiwa. Shambhu Lal muumini wa dhehebu la Hindu anatuhumiwa kumuua mtu huyo na kutuma picha katika mitandao ya kijamii. Polisi inasema zaidi ya watu mia saba wamechangia akaunti yake. Video hiyo inamuonyesha Shambhu Lal akimlazimisha mtu huyo kuingia dhehebu la Kihindu kabla ya baadae kutuma picha akiwa amefariki.

Dereva aliyesababisha ajali ya gari la shule kuhojiwa Ufaransa

Image
Image caption Ajali hiyo ilitokea karibia na eneo la shule Wapelelezi nchini Ufaransa wanasubiria kumuhoji mwanamke dereva wa gari la shule lililogonga treni karibu na Perpignan Mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watoto wanne. Amepata majeraha kadhaa. Waziri mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe aliyekwenda eneo la tukio amesema watu 11 wapo katika hali mbaya. Wengine tisa walijeruhiwa kidogo. Amesema kazi ya kuwatambua majeruhi imekua ngumu. Gari hilo lilikuwa ndio limepakiwa wanafunzi hao muda mfupi na lilitembea mwendo wa kilomita moja tu kabla ya ajali hiyo.

Tanzania yajitenga na Trump kuhusu Jerusalem

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Mji wa Jerusalem una maeneo matakatifu kwa Waislamu, Wakristo na Wayahudi Tanzania imesema haikubaliani na hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kupitia taarifa imesema nchi hiyo inaunga mkono makubaliano ya kimataifa ambayo yanatambua haki ya watu wa Palestina kumiliki Mashariki mwa Jerusalem kama ilivyokuwa kwenye mpaka wa kabla ya mwaka 1967. "Tanzania inaunga mkono msimamo wa Umoja wa Mataifa wa suluhu ya mataifa mawili ambayo unatoa nafasi ya Israel na Palestina kuwepo kwa pamoja zikiwa na mipaka salama," taarifa hiyo iliyotuwa saini na Waziri Augustine Mahiga imesema. Bw Trump kando na kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel, alisema nchi hiyo pia itahamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv. Bw Mahiga amesema ubalozi wa Tanzania utaendelea kuwepo mjini Tel Aviv. Msimamo wa Tanzania unaenda sambamba na msimamo wa mataifa mengi ...