Posts
Showing posts from September 24, 2017
FIESTA MWANZA: Alikiba alivyoliamsha live na wimbo wa ‘Mwana’ (+video)
- Get link
- X
- Other Apps
“Walitishia kutupiga risasi wakachukuwa ng’ombe wetu” – Wanakijiji
- Get link
- X
- Other Apps
Wanikijiji wa Ololosokowani katika Wilaya la Ngorongoro, akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji Kerry Dukanyi wameiomba Serikali kuingilia kati zoezi la mnada wa ng’ombe 630 bila kufuata taratibu wakidaiwa kuingia kwenye hifadhi. Baadhi ya wanakijiji hao wameeleza kusikitishwa na kitendo kilichofanywa kukusanya mifugo yao ambayo wanasema ilikuwa ndani ya mipaka ya kijiji kisha kupigwa mnada huku wengine wakisema kabla ya kuchukuliwa kwa ng’ombe hao walitishiwa kupigwa risasi.
Tetesi za soka Ulaya Jumapili 24.09.2017
- Get link
- X
- Other Apps
Image caption Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ameanza harakati za kutaka kusaini kandarasi mpya na Aaron Ramsey na Danny Welbeck Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ameanza harakati za kutaka kusaini kandarasi mpya na Aaron Ramsey na Danny Welbeck akiongezea kuwa anatarajia wachezaji wengine kukamilisha kandarasi zao. Kandarasi za wawili hao zinakamilika 2019.(Guardian) Real Madrid wanamchunguza mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane kwa lengo la kumsajili via Daily Express) Image caption Real Madrid wanamchunguza mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane kwa lengo la kumsajili via Daily Express) Chelsea inaongoza Liverpool, Tottenham, Southampton, Manchester City na Manchester United katika kumsaka kinda Elye Wahi, 14, ambaye tayari ameanza kuifungia klabu ya Caen ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 na anatoka katika mtaa wa Courcouronnes, makaazi ya Paris ambayo kiungo wa kati wa Chelsea N'Golo Kante anatoka. (Sun) Arsenal wana mpango wa ku...
Chelsea, Man United, Man City na Tottenham zawika
- Get link
- X
- Other Apps
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Alvaro Morata alifungia Chelsea mabao matatu dhidi ya Stoke City Hat-trick ya Alvaro Morata imeisaidia Chelsea kuicharaza Stoke City na kuongeza rekodi ya ushindi wao msimu huu. Kikosi cha Antonio Conte kilichukua uongozi baada ya dakika mbili pekee, huku Morata akionyesha umahiri wake kwa kufunga krosi ya Cesar Azpilicueta na kumwacha kipa Jack Butland bila jibu. Stoke iliizawadi Chelsea bao la pili wakati nahodha Darren Fletcher aliyempatia pasi mbaya kipa kabla ya Pedro kuingilia kati na kucheka na wavu. Mshambuliaji Alvaro Morata alifunga bao la tatu baada ya kutamba na mipira akiwa amesalia na nusu ya uwanja kabla ya kuongeza bao lake la tatu na la nne maguu sita ndani ya eneo hatari. Ilikuwa mchezo mzuri kwa Chelsea ambao walifunga mashambulio yao yote. Wakati huohuo viongozi wa ligi Manchester City walilazimika kusubiri kabla ya kuwashinda nguvu Crystal Palace ambao hadi kufikia sasa hawajapata bao ama alama hata m...
Rais Magufuli awatunuku kamisheni maafisa 422 wa jeshi
- Get link
- X
- Other Apps
Haki miliki ya picha IKULU YA RAIS TANZANIA Image caption Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua paredi ya maafisa wapya kundi la 61/16 kabla ya kuwatunuku kamisheni kuwa maafisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Uwanja wa shekhe Amri Abeid Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni maafisa wapya 422 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Maafisa hao wametunukiwa cheo cha Luteni Usu ambapo 314 kati yao walihitimu katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Mkoani Arusha, 84 wakihitimu mafunzo katika shule ya ubaharia ya kijeshi, 14 wakiwa wamehitimu mafunzo katika shule ya urubani ya kijeshi na 10 wakiwa wameiitimu mafunzo ya kijeshi nje ya nchi. Akizungumza baada ya kuwatunuku kamisheni hizo rais Magufuli amewapongeza maafisa hao na kuwataka kuendelea kulitumia Taifa kwa kuzingatia kiapo chao. Amesema kuwa jeshi la ulinzi limefanya kazi kubwa kulinda mipaka na kukabiliana na vitisho ...
Iran yafanyia majaribio kombora lake
- Get link
- X
- Other Apps
Image caption Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr. Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr. Kombora hilo lilionyeshwa hadharani katika maonyesha ya kijeshi jana Ijumaa. Iran imesema kuwa kombora hilo linaweza kusafiri mwendo wa kilomita 2,000. Kituo cha runinga cha taifa hilo kilionyesha picha za sherehe hizo. Kombora la kwanza la Khorram-Shahr lilirushwa angani Januari lakini likalipuka katikati ya mwendo. Image caption Rais Donald Trump na rais Rouhani wa Iran Jaribio hilo lilifanywa siku chache baada ya Rais Trump wa Marekani kushambulia Iran katika hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Rais wa Iran, Hassan Rouhani, ametetea hatua ya taifa lake kuimarisha zana zake kwa lengo la kujitetea.
Marekani na korea zazidi kuoneshana ubabe.Ndege za kijeshi za Marekani zapaa karibu na Korea Kaskazini kuonyesha ubabe
- Get link
- X
- Other Apps
Image caption Ndege za kijeshi za Korea Kaskazini zapaa karibu na anga ya pwani ya Korea Kaskazini kuonyesha ubabe Ndege za kijeshi za Marekani zimepaa karibu na pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini katika kuonyesha ubabe wa kivita, idara ya ulinzi nchini Marekani pentagon imesema. ''Hatua hiyo ni kuonyesha kuwa rais Trump ana njia tofauti za kijeshi kushinda vitisho vyovyote'' , msemaji Dana White alisema. Marekani na Korea Kaskazini zimerushiana cheche za maneneo katika kipindi cha hivi majuzi. Katika Umoja wa mataifa siku ya Jumanne, bwana Trump alisema kuwa ataiangamiza Korea Kaskazini iwapo Marekani italazimika kujitetea na washirika wake. ''Hili ni eneo ambalo jeshi lolote halifai kupitia na ni ndege za kijeshi za Marekani ambazo zimeweza kulifikia katika karne ya 21, licha ya tabia mbaya ya Korea Kaskazini'', alisema Bi White. Tangazo hili lilijiri muda mfupi kabla ya waziri wa kigeni wa Korea Kaskazini kutoa hotuba yake ka...