Posts

Showing posts from August 7, 2017

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUIFANYA NYUMBA YAKO KUWA BORA NA SALAMA

Image
Habari za siku rafiki, ni tumaini langu kuwa bado unaendelea kuweka juhudi na maarifa kuhakikisha unafikia malengo ambayo umejiwekea mwaka huu. Hilo ni jambo nzuri na hongera kwa kila hatua ambayo umefanikiwa kuifikia. Karibu tena kwenye Makala hii tuendelee kushauriana mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo na uwekezaji wa ardhi na majengo. Katika safari hii wapo baadhi ya marafiki wanapitia changamoto mbalimbali zinazohusiana na uwekezaji huu kutokana na sababu mbalimbali ambazo wengi wao ni kwa sababu ya kukosa maarifa sahihi. Leo nitazungumzia mambo muhimu ya kuzingatia ili kuifanya nyumba yako kuwa bora na salama wakati wote. Hapa nazungumzia uimara wa nyumba kuweza kumudu mazingira kwa muda mrefu pasipo kufanyiwa marekebisho yasiyo na ulazima wowote. Nyumba ni matokeo ya ubunifu na usanifu wa mambo mbalimbali ambayo yanatimiza kiu ya matumizi, ubora na mwonekano uliopo. Ili kuyatimiza haya yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa kabla ya ujenzi, wakati wa ujenzi na baada ya ujenzi ili ...