Posts

Showing posts from September 16, 2017

Morgan Tsvangirai apelekwa Afrika Kusini kwa matibabu

Image
Image caption Morgan Tsvangirai apelekwa Afrika Kusini kwa matibabu Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, amepelekwa Afrika Kusini kwa matibabu. Wafuasi wa chama chake cha MDC, wanasema hali yake siyo mbaya sana, na inatokana na kujituma sana. Mwaka jana, Bwana Tsvangirai alipatikana na saratani. Mwandishi wa BBC nchini Zimbabwe, anasema watu wengi wanauliza, iwapo Bwana Tsvangirai, ni mzima vya kutosha, kuweza kuongoza muungano wa upinzani, dhidi ya Rais Robert Mugabe, katika uchaguzi wa mwaka ujao. Rais Mugabe, mwenye umri wa miaka 93, ameiongoza Zimbabwe tangu mwaka wa 1980.

PRODUCER EMA THE BOY AMEPOTEA HAJULIKANI ALIPO

Image

SPIKA NDUGAI AWATAHADHARISHA WABUNGE KUHUSU USALAMA WAO

Image
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai amewataka Waheshimiwa Wabunge kuchukua tahadhari juu ya usalama wao mahali popote wanapokuwa ili kujiepusha na matukio ya kihalifu yanayotokea hapa Nchini. Spika Ndugai ametoa tahadhari hiyo jana Bungeni Mjini Dodoma baada ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Kasim Majaliwa Majaliwa kutoa hoja ya kuahirisha Mkutano wa Nane wa Bunge. “Tuchukue hatua katika maisha yetu, kama mnavyosikia matukio ni mengi katika Nchi yetu, usalama unanza na wewe kwanza halafu vyombo vya ulinzi vinavyotulinda vinasaidia tu kidogo, tutazame nyendo zetu,”  alisema. Aidha, Mheshimiwa Ndugai amewaomba Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki Mheshimiwa Tundu Lissu pamoja na wale wanaomuuguza wakiwemo waheshimiwa Wabunge. Vilevile Meshimiwa Spika amewapangia Kamati Waheshimiwa Wabunge wapya wanane(8) wa Chama cha Wananchi (CUF) walioapishwa katika Mkutano huu wa Nane wa Bunge. Wajumbe hao na Kamati zao ni Mheshimiwa Shamsia Mtamba...

Wanaharakati wakwama mahakamani sakata la wanafunzi wajawazito kuondolewa shuleni

Image
Takwimu za 2007 zinaonyesha Mkoa wa Mtwara uliongoza kwa wanafunzi 435 kuacha shule kutokana na ujauzito.  Kwa ufupi DONDOO Takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinaonyesha tangu 2004 hadi 2008, wastani wa wanafunzi wa kike 5,720 nchini wanaacha shule kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo ujauzito. Takwimu za 2007 zinaonyesha Mkoa wa Mtwara uliongoza kwa wanafunzi 435 kuacha shule kutokana na ujauzito.  Mikoa iliyofuata na idadi ya wanafunzi waliopata ujauzito katika mabano ni Mwanza (308), Tanga (290), Pwani (280), Rukwa (265), Ruvuma (204), Lindi (144), Shinyanga (137), Dodoma (111) na Mbeya (105). By James Magai, Mwananchi jmagai@mwananchi.co.tz Dar es Salaam. Jitihada  za wanaharakati kutetea wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni kuendelea na masomo baada ya kujifungua zimegonga mwamba kutokana na Mahakama Kuu kukubaliana na Kanuni za Elimu za mwaka 2002, zinazozuia wanafunzi hao kuendelea na masomo. Uamuzi huo wa ...

Serikali Yaapa Kupambana na Wanaojihusisha na Mapenzi ya Jinsi Moj

Image
Serikali imesema inapambana kwa nguvu zote na vitendo vya mapenzi ya jinsi moja na kwamba, mwanamume atakayethibitika kufanya vitendo vya kike ataadhibiwa kisheria. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla alisema hayo jana Ijumaa alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Susan Lyimo. Mbunge huyo alisema kumekuwa na biashara kati ya wanaume na wanawake lakini pia ipo ya watu wa jinsi moja. “Nataka kufahamu hao wanachukuliwa hatua gani?” alihoji Lyimo. Naibu waziri alisema sheria inakataza watu wa jinsi moja kufanya mapenzi  kinyume cha maumbile na pia inakataza wanaume kufanya vitendo vya jinsi ya kike. Alisema kuna adhabu kali hutolewa na sheria hiyo kwa mtu anayebainika kufanya vitendo hivyo na kwamba, adhabu yake ni kifungo cha hadi zaidi ya miaka 30 jela. “Tumekuwa tukipambana kwa nguvu zetu zote na makundi haya ambayo yamekuwa yakishiriki katika vitendo vya mapenzi ya jinsi moja, kuyahamasisha ama ...

Tevez namba 1 kwa kulipwa mshahara mkubwa duniani, Kocha kataja sababu za kutomchezesha

Image
Inawezekana taarifa hizi zikakushangaza kwa sababu imekuwa kawaida kwa kuona mchezaji mwenye uwezo mkubwa duniani akilipwa mshahara mkubwa, taarifa zilizoripotiwa kutoka  China  zinaeleza kuwa  Carlos Tevez ambaye ni mchezaji namba moja duniani kwa kulipwa mshahara mkubwa kocha mpya havutiwi nae. Kocha mpya wa club ya  Shanghai Shenhu  ya  China   Wu Jingui   havutiwi na uwezo wa  Carlos Tevez  na ameanza kumuweka benchi, kitendo ambacho wengi wanahisi staa huyo atarudi tena kwao  Argentina  katika dirisha la usajili la January baada ya kocha wao mpya kuonesha kutohitaji huduma yake. “Kwa sasa siwezi kumchezesha kwa sababu hayupo fiti physically, hayuko fiti kucheza, amezidi uzito, kama kwa kiasi kikubwa huwezi kucheza kwa kiwango hakuna point au ulazima wa mimi kukupanga, nimefundisha mastaa wengi wa kubwa lakini sikuwahi kuwapanga kwa sababu ya majina yao tu”>>> Wu Jingui Tevez   ambaye an...

NOMA !! Mapokezi ya Diamond Platnumz Mozambique

Image
Mwimbaji wa Bongofleva  Diamond Platnumz  alikwenda  Mozambique  kwa ajili ya kutumbuiza kama kawaida ambapo hii video inaonyesha sehemu tu ya mapokezi yake kuanzia alipowasili uwanja wa ndege. Na Ayo Tv

Makubwa ya Magazeti ya TZ leo September 16.. Udaku, Michezo na Hardnews

Image
Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo September 16  2017  kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa

Tanzania yashangazwa na uchunguzi wa UN kuhusu Korea Kaskazini

Image
Image caption Dkt Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Tanzania Tanzania imesema imeshtushwa baada ya kuorodheshwa miongoni mwa nchi ambazo zimechunguzwa na Umoja wa Mataifa na kuhusishwa kuwa na uhusiano wa kibiashara na Korea Kaskazini. Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, waziri wa mambo ya nje Dkt. Augustine Mahiga, amesema licha ya uhusiano uliokuwepo awali, lakini tangu mnamo mwaka 2014, Tanzania imepunguza kabisa uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na nchi hiyo. "Hatuna ugomvi na Korea Kaskazini,lakini kitendo chao cha kutengeneza masilaha ya kuangamiza sio mazuri kwa heshima na usalama duniani.Ndiyo maana tukaanza kuchukua hizo hatua za kupunguza mahusiano." amesema Dr Mahiga kwa waandishi wa habari leo. Waziri Mahiga ameongeza kusema kuwa, uhusiano huo wa kibiashara ulikuwepo kabla ya vikwazo vilivyowekwa hivi karibuni na Baraza la Umoja wa Mataifa. Waziri huyo amesema anaelekea katika mkutano wa kawaida wa Um...