Uamuzi kuhusu kesi ya uchaguzi wa urais Kenya
Mahakama ya Juu nchini Kenya leo inatoa uamuzi kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi uliopita ambayo iliwasilishwa na muungano wa upinzani National Super Alliance. Tume ya uchaguzi ilimtangaza Rais Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi huo uliofanyika tarehe 8 Agosti Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo akiwa na kura 8,203,290 (54.27%) Tume ya uchaguzi ilisema Raila Odinga alipata kura 6,762,224 (44.74%) Upinzani unadai mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa na kuingiliwa kumfaa Rais Kenyatta. Wakati wa kusikizwa kwa kesi, kulikuwa na mvutano kuhusu kukaguliwa kwa mitambo ya tume ya uchaguzi Mahakama ya Juu inaweza kuidhinisha au kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi. Iwapo ushindi wa Rais Kenyatta utaishinishwa, basi ataapishwa Septemba 12 Iwapo uchaguzi utafutiliwa mbali, uchaguzi mwingine utafanyika katika kipindi cha siku 60