Kikombe kimoja cha kahawa kwa siku chapunguza hatari ya ugonjwa wa moyo
Mbali na faida kemkem tunazozijua zinazopatikana kwenye kahawa, utafiti mpya umesema kwamba kunywa kikombe kimoja tu cha kahawa kwa siku kunapunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo. Utafiti huo uliotolewa katika Kongamano la Jumuiya ya Mshituko wa Moyo la Kimataifa nchini Marekani, umeeleza kwamba kunywa kikombe kimoja cha kahawa ya kawaida na isiyokuwa na kafeini kila siku huzuia kupatwa na mshituko wa moyo kwa asilimia 30. Hata hivyo wataalamu wameonya kuwa kutumia sana kinywaji hicho matokeo yake huweza kuwa kinyume. Tafiti za huko nyuma pia zilionyesha kuwa, kunywa kila siku kahawa kunaweza kumzuia mtu asipate kisukari aina ya pili na ugonjwa wa akili. Mpenzi mdau baada ya kufahamu hayo, nimeonea nichukue fursa hii kuelezea baadhi ya faida za kahawa. Mbali ya kawaha kuwa kinywaji murua ambacho kinaweza kukufanya uchangamke asubuhi baada ya kuamka, au kwa wale kina yakhe wanaopenda kuburudika kwa kunywa kahawa kwa kashata vijiweni au kando ya barabara huk...