Posts

Showing posts from November 19, 2017

Waandamanaji wapiga kambi nje ya makao ya Mugabe

Image
Image caption Waandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu. Waandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu. Maandamano hayo yanajiri kufuatia furaha ilioonekana miongoni mwa raia baada ya jeshi kuingilia kati na kumzuia rais Mugabe kwa muda nyumbani kwake siku ya Jumatano. Wanajeshi katika ikulu ya Whitehouse walioonekana wakiwarudisha nyuma waandamanaji. Jeshi liliingilia kati baada ya rais Mugabe kumfuta kazi makamu wake wa urais , akionyesha ishara za kutaka mkewe kumrithi. Image caption Waandamanaji wakiunga mkono jeshi Bwana Mugabe , mwenye umri wa miaka 93 ameiongoza Zimbabwe tangu ilipojipatia uhuru kutoka kwa Uingereza 1980. Jeshi limehakikisha kuwa anaendelea kukaa katika makoa yake huku likidai kujadiliana naye na kwamba litatangaza kwa wananchi matokeo ya mazungumzo hayo hivi karibuni. Mkutano wa siku ya Jumamosi unaungwa mkono na jeshi na wanachama wa chama cha Zanu ...

MAGAZETI YA TZ NA NJE LEO NOVEMBA 19,2017

Image

Aliyetajwa kufariki dunia ajali ya ndege Ngorongoro, yupo hai

Image
Muhina ambaye ni mwongozaji watalii katika hoteli hiyo, alikuwa aondoke na ndege ya Coastal Aviation saa nne asubuhi lakini viongozi wa hoteli walimbadilishia ndege, hivyo aliondoka na Air Exel iliyofika salama Serengeti. Arusha. Mfanyakazi wa hoteli za kitalii za andBeyond Serengeti, Moses Muhina aliyetajwa kuwa ni miongoni mwa abiria waliofariki dunia katika ajali ya ndege ya Shirika la Coastal Aviation, imebainika alibadili ndege muda mfupi kabla ya safari ili kuwahi kazini. Muhina ambaye ni mwongozaji watalii katika hoteli hiyo, alikuwa aondoke na ndege ya Coastal Aviation saa nne asubuhi lakini viongozi wa hoteli walimbadilishia ndege, hivyo aliondoka na Air Exel iliyofika salama Serengeti. Akizungumza na gazeti hili, meneja uendeshaji wa Hoteli ya andBeyond Serengeti Under Canvas, Mussa Matala alisema Muhina ambaye anasomeka kwenye orodha ya ndege kama Maina alikuwa apande ndege hiyo lakini walimbadilishia. Alisema waliomba aondolewe kwenye orodha ya wasafir...

Real Madrid yabanwa mbavu, Barcelona yajikita kileleni ‘La Liga’

Image
Klabu ya Real Madrid jana usiku imelazimishwa sare ya bila kufungana na mahasimu wao klabu ya Atletico Madrid kwenye mchezo wa Ligi kuu nchini huu ‘La Liga’. Mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa ilionekana timu zote kutoshana nguvu kwani kipindi cha kwanza Madrid walionekana kutawala mchezo huku Atletico wakitawala kipindi cha pili. Hii inakuwa ni mara ya kwanza Real Madrid kutoka sare tasa ya bila goli ugenini kwa mechi 35 iliyocheza chini ya Kocha Zinedine Zidane. Kwaupande mwingine watani wao wa jadi, FC Barcelona hao walipata ushindi mnene wa goli 3-0 dhidi ya klabu ya Leganes na kuifanya klabu hiyo kujikita kileleni kwa alama 10 zaidi ya klabu za Madrid na Atletico.

UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA

Image
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amezindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, utakaogharimu shilingi bilioni 10 zilizotolewa na Benki ya Dunia. Lengo la utafiti huo utakaofanywa na Ofisi Kuu ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni kupata takwimu zinazohusu shughuli za kijamii na kiuchumi, mapato na matumizi, hali ya makazi na umiliki wa rasilimali katika ngazi ya kaya. Dkt. Mpango alisema kuwa  Utafiti huo utaiwezesha Serikali kupima kiwango cha hali ya umaskini wa kipato, chakula na pengo baina ya matajiri  na maskini kuanzia kipindi cha mwaka 2013 hadi sasa. “Takwimu zilizopo hivi sasa zinaonesha kwamba kiwango cha umasikini wa kipato ulipungua kutoka asilimia 34 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 28.2 mwaka 2012” Alisema Dkt. Mpango. Alisema pamoja na takwimu hizo, bado kiwango cha umasikini ni kikubwa na kwamba Serikali kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimb...