Posts

Showing posts from September 9, 2017

Madaktari watoa meno 7 kutoka kwa mtoto wa mwezi mmoja India

Image
Image caption Madaktai watoa meno 7 kutoka kwa mtoto wa mwezi mmoja India Madaktari kwenye hospitali moja iliyo jimbo la magharibi mwa Inida ya Gujarat wamefanikiwa kutoa meno saba kutoka kwa mtoto wa mwezi mmoja. "Kwa sasa mtoto yuko sawa," daktari ambaye alifanya upasuaji huo Meet Ramatri alisema. Alisema kuwa upasuiji huo ulifanya kwa njia mbili. Kwanza walitoa meno manne, na baadaye matatu. Meno ya mtoto huyo yaligundulwia siku chache baada ya kuzaliwa. Wazazi wake walimpeleka kwa daktari wakati alipata matatizo ya kunyonya, Image caption Madaktai watoa meno 7 kutoka kwa mtoto wa mwezi mmoja India Baada ya kumfanyia uchunguzi dakari aligundua nyama nyeupe na kumtuma kwa daktari Ramatri. "Wakati nilimfanyia uchunguzi aligundua meno saba," Dr Ramatri aliambia BBC. Kisha alilazimika kutoa meno hayo kwa njia ya upasuajia. "Sasa mtoto huyo anaweza kunyonya," dakatari alisema, lakini aliongeza kuwa ni vigumu kujua ikiwa upasuaji huo ...

Gwiji wa muziki wa country Don Williams afariki dunia

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Don Williams alianza kuimba muziki kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971 Mwanamuziki nyota wa nyimbo za mtindo wa country kutoka Marekani Don Williams amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78. Mzaliwa huyo wa jimbo la Texas amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi, afisa anayesimamia mawasiliano yake ametangaza. Williams alianza kuimba nyimbo kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971, na tangu wakati huo alichomoa nyimbo 17 zilizogonga chati za muziki wa country. Nyimbo zake zilizovuma zaidi ni pamoja na  Gypsy Woman  na  Tulsa Time , ambazo ziliimbwa tena na wanamuziki wengine kama vile Eric Clapton na Pete Townshend. Williams alitazamwa na wengi kama gwiji mnyenyekevu wa muziki wa country. Nyimbo zake nyingine zilizovuma ni pamoja na  You're My Best Friend, I Believe in You  na  Lord, I Hope This Day Is Good . Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Troy Gentry alikuwa amepang...

Kimbunga Irma chawasili Cuba

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Kimbunga Irma kikiandamana na upepo mkali. Kimbunga hicho ambacho kimeendelea kuimarika saa chace zilizopita kinatarajiwa kuathiri miji ya pwani. Kifikia sasa watu ishirini wamerikpotiwa kufariki katika visiwa vya Carebean. Msemaji wa kituo cha kushughulikia majanga, nchini Marekani,amesema kimbunga hicho huenda kika-muangamiza mtu yeyeyote ambaye hatajiepusha nacho.  Kumeshuhudiwa msongamano mkubwa wa magari na upungufu wa petroli, wakaazi wa Florida wakielekea maeneo ya kaskazini. Wakati huo huo kimbunga Ema kinachoendelea kusonga kwa kasi,sasa kimeingia nchini Cuba.  Kimbunga hicho, kinaandamana na upepo mkali na mvua kubwa kuelekea visiwa vya kaskazi mwa Caribbean. Bahamas hata hivyo imenusurika na kimbunga hicho baada ya upepo kubadilisha mkondo. Visiwa vya mashariki vilivyokuwa vimekumbwa na mafuriko makubwa sasa ya yanakabiliwa na tishio la kugongwa na kimbunga kingine. Shughuli ya kuwaondoa watu kati...