Posts

Showing posts from November 27, 2017

Southampton 4-1 Everton

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Southampton imekwea hadi nafasi ya 10 kwenye orodha ya ligi baada ya kuishinda Everton. Matatizo ya Everton chini ya meneja David Unsworth yameendelea kudhihirika wakati wamedidimia katika Ligi ya England kwa kushindwa pakubwa na Southampton. Mshambuliaji wa Saints, Charlie Austin amefunga magoli mawili kwa kichwa katika nusu ya pili ya mechi hiyo, baada ya Dusan Tadic kuwapa wenyeji Southampton uongozi wa mapema. Mchezaji wa Everton aliyelipiwa gharama ya juu kuliko mchezaji mwingine katika klabu hiyo Gylfi Sigurdsson alisawazisha mambo kabla ya kipenga cha mapumziko lakini Southampton wakafyetuka kwa kasi baada ya mapumziko hayo. Baada ya magoli mawili ya Austin, Steven Davis alimchenga Jordan Pickford kutoka ukiongoni mwa boxi kuufunga ushindi kwa Saints, ambaop waliwahi kufunga magoli sita ya msimu huu nyumbani kabla ya mechi ya leo.

Bao la lala salama laipa Arsenal ushindi

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Alexis Sanchez amefunga bao lake la nne msimu huu na kuipa Arsenal ushindi Alexis Sanchez amefunga penalti katika muda wa kuyoyoma na kuipa Arsenal ushindi dhidi ya Burnley uwanjani Turf Moor. Ilikuwa ni marudio ya mechi ya msimu uliokwisha kati ya timu hizo mbili uwanjani Emirates wakati raia wa Chile - Sanchez alipofunga bao kunako dakika 98 kushinda mechi hiyo. Ilikuwa pia ni mara ya tatu mtawalia kuwa Gunners imepata ushindi katika muda wa mwisho wa mechi dhidi ya Clarets. Pointi tatu iliyojinyakulia Arsenal inaikweza timu hiyo hadi katika nafasi ya nne kwenye orodha wakati wakisubiria mechi yao dhidi ya wapinzani wao wa Londona kaskazini Tottenham, waliotoka sare ya 1-1 dhidi ya West Brom Jumamosi. Matokeo hayo yalikuwa ni kipigo kwa upande wa Sean Dyche ikiwa wamefanikiwa ushindi wa mechi zao mpaka sasa ikiwa walionekana kama watanyakuwa japo pointi moja, kabla ya refa Lee Mason kuashiria sehemu ambapo mlinzi James Ta...

Ufaransa yaichapa Ubelgiji, yashinda kombe la Davis

Image
Image caption Wachezaji wa Ufaransa wakishangilia ushindi Ufaransa imefanikiwa kushinda kombe la Davis kwa mara ya kumi katika historia baada ya kuichapa Ubelgiji katika mchezo wa fainali. Ufaransa walianza kwa ukali na kuongoza kabla ua Ubelgiji kusawazisha kupitia David Goffin lakini Ufaransa ikaongeza makali na kushinda kwa seti 7-6 (7-5) 6-3 6-2. Ni michuano ambayo watu wengi walidhani Ubelgiji ingejizolea taji hilo kutokana na uonyesha kiwango safi kwa msimu huu. Mara ya mwisho mwa Ufaransa kushinda taji hili ilikuwa mwaka 2001, na kwa ushindi huu umati mkubwa wa watu 27,000 walijitokea kushangilia kwa kila aina katika uwanja wa Lille.

Mugabe 'anaendelea vizuri' baada ya kujiuzulu

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Alikuwa ni mtu aliyependa sherehe kubwa ambazo zilikuwa zikiandaliwa mara kwa mara na chama tawala cha Zanu-PF Mpwa wa Robert Mugabe anasema kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe ana raha na afya njema licha ya kulazimishwa kujiuzulu wiki hii baada ya kutawala kwa miaka thelathini na saba. Leo Mugabe ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, kwamba alimtembelea mjombake ambaye anasema anaendelea vizuri baada ya utimuliwa kwake madarakani. Kauli ya Leo Mugabe inaashiria kiongozi huyo mkongwe amezoea kwa upesi kutimuliwa kwake kutoka uongoai wa taifa hilo. Amesema mjombake anatazamia maisha yake ya baada ya uongozi, ambayo yatajumuisha ukulima na kuishi katika nyumba yake mashambani. 'Grace, bado yupo naye' amesema Leo Mugabe akimaanisha mkewe rais huyo wa zamani.  Ameeleza kuwa anashughulika na mipango ya kujenga chuo kikuu kwa heshima ya mumewe ili kuwapa shughuli ya kufanya. Hatahivyo, taarifa katika gazeti la Zimbabw...

Wanasayansi: Ziwa Victoria lipo hatarini kukauka

Image
Image caption Muonekano wa ziwa Victoria Wanasayansi wanasema kwamba ziwa kubwa zaidi lenye maji tulivu barani Afrika Victoria linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka. Wanasema kwamba uvuvi haramu na uliopitiliza pamoja na uvamizi wa mazingira kuzunguka maeneo ya ziwa ni sababu kubwa. Maji machafu pia yanayotiririshwa kuelekea kwenye ziwa yanahatarisha usalama wa viumbe vya majini. Mwandishi wa BBC anasema jeshi la Uganda limeweka mipango maalum ikiwa ni pamoja na kuharibu nyenzo za uvuvi zinazotajwa kuwa miongoni mwa sababu.

Hatari yaongezeka kwa mlima wa volkano kulipuka Bali

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Maafisa wanasema mlma huo wa volkano umekuwa ukitoa moshi mkubwa mfululizo Mamlaka nchini Indonesia imetangaza hali ya tahadhari kubwa kufuatia kuwepo dalili za kutokea mlipuko mkubwa wa Volcano katika mlima wa Agung.  Uwanja wa ndege wa kipekee katika kisiwa hicho maarufu cha utalii cha Bali umefungwa. Majivu na moshi wa Volcano hiyo imefikia urefu wa zaidi ya mita 3000 juu ya mlima huo hali iliyosababisha giza. Mlima huo uitwao Agung ulirusha majivu mengi na kutandaza mvuke na moshi mwingi mara ya pili katika kipindi cha wiki moja.  Maafisa wamehimiza na kuwasaidia maelfu ya wakaazi na watalii kulihama ene hilo na kwenda kwingine. Mwaka 1963 mlima huo ulilipuka na kusababisha vifo vya takriban watu 1,600.