Msuva Azikana Taarifa za kuwa Amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mwezi
WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amecheza kwa dakika zote 90 timu yake, Difaa Hassan El - Jadida ikilazimishwa sare ya 0-0 na Ittihad Tanger katika mchezo wa Kombe la FA Morocco Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan. Akizungumza, Msuva alisema kwamba walikuwa wana mechi ngumu jana kwa sababu walikutana na wapinzani wazuri. “Ilikuwa mechi ngumu sana, jamaa wazuri sana, lakini tutajitahidi tushinde mechi ya marudiano kwao tusonge mbele,”alisema Msuva. Mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola kati ya Difaa Hassan El – Jadida na FUS Rabat uliokuwa ufanyike leo Uwanja wa FUS, Hay Nahda mjini Rabat umeahirishwa. Difaa sasa watasafiri kuifuata Ittihad Tanger Septemba 20 kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la FA. Wakati huo huo: Simon Msuva amekanusha uvumi kwamba yeye ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa klabu yake, Difaa Hassan El- Jadida. “Kaka hizi habari mimi sijui hata zinatoka wapi, ha...