Posts

Showing posts from September 6, 2017

Serikali yakanusha ugonjwa wa Ebola kuwepo nchini

Image
Serikali imekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii za kuwepo ugonjwa wa Ebola nchini zinazodai kuwa ugonjwa huo umeingia nchini kupitia nchi jirani ya Rwanda.

BREAKING NEWS: Viongozi wa Nne wa CUF Wanaomuunga Mkono Lipumba Wamefariki kwa Ajari

Image
Stori iliyonifikia asubuhi hii ya Jumatano September 6, 2017 ni kwamba Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi CUF wanaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba wamefariki dunia baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani. Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati Viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho baada ya gari lao kugongana na Lori. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa CUF Abdallah Kambaya Viongozi waliofariki ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao ni Mgombea Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahmika kwa jina moja Uredi. Aidha, idadi ya majeruhi haijajulikana ila ni hawazidi 10 na baadhi yao wapo Hospital ya Tumbi huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni gari la wafuasi hao kugongana na lori.

Watu wafanya maandalizi ya mwisho kabla kuwasili kimbunga Irma

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Watu wafanya maandalizi ya mwisho ya kuwasili kimbunga Irma Visiwa vilivyo eneo la Caribbean vimefanya matayarisho ya mwisho kwa kimbunga Irma, ambacho ni kimbunga chenye nguvu zaidi kwa mwongo mmoja, huku maafisa wakionya kuwa kimbunga hicho kinaweza kuwa chenye madhara makubwa. Haki miliki ya picha EPA Image caption Watu wafanya maandalizi ya mwisho ya kuwasili kimbunga Irma Kimbunga Irma cha kiwango cha tano kimepata nguvu ya upepo wa kasi ya hadi kilomita 295 kwa saa. Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga visiwa vya Leeward kabla ya kuelekea huko Puerto Rico, Haiti na Floirda. Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Watu wafanya maandalizi ya mwisho ya kuwasili kimbunga Irma Watu wameamrishwa kuondoka kwa lazima eneo la magharibi mwa Florida. Wageni watatakiwa kuondoka Jumatano asubuhi huku wenyeji nao wakitakiwa kunodoka ifikapo jioni na safari zote za ndege kusitishwa. Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Watu...