Posts

Showing posts from September 5, 2017

Diego Simeone ajifunga Atletico Madrid mpaka 2020

Image
Image caption Simeone ameibuka kuwa lulu ndani ya klabu ya Atletico Madrid Kocha wa Klabu ya Atletico Madrid Diego Simeone amezima tetesi za kuhamia klabu ya Inter Milan ya Italia baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea kufundisha miamba hiyo ya jiji la Madrid. Murgentina huyo alikuwa akihusishwa na kuhamia kwa vigogo hao wa Italia, ambao aliwachezea kuanzia mwaka 1997 hadi 1999, lakini ameamua kujifunga na waajiri wake wa sasa. Simeone anapendwa sana na mashabiki wa Atletico Madrid ambao wamejenga imani kubwa kwake kufuatia kushinda taji la La Liga kama mchezaji na baadaye kocha. Simeone amesaini mkataba mpya ambao unamfunga Atletico Madrid kwa misimu miwili zaidi, mpaka Juni 30, mwaka 2020 .

La Liga yaishitaki Ma city, matumizi makubwa ya fedha

Image
Image caption Man City imekuwa na mabadiliko makubwa tokea kuchukuliwa na wamiliki wa Abu Dhabi mwaka 2008 Shirikisho la soka nchini Hispania (La Liga) limeliandikia barua shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) wakitoa malalamiko kuhusu ukiukwaji wa sheria za matumizi Financia Fair Play (FFP) unaofanywa na klabu ya Man City. Raisi wa La Liga Javier Tebas alitoa malalamimo kuhusu wamiliki wa klabu ya Manchester City ambao pia ni wamiliki wa klabu ya PSG kutokana na matumizi makubwa ya kifedha wanayoyafanya. Image caption Kuwasili kwa Neymar PSG kunatajwa pia kuwa sababu Lakini baadaye shirikisho la soka la UEFA lilitoa majibu kuhusiana na barua iliyoandikwa na Rais wa La Liga kwa kusema kwamba shirikisho hilo halitaichunguza klabu hiyo na taarifa nyingine kinyume na hapo ni uongo.

Polisi wachunguza vifo vingi vya watoto wanaozaliwa India

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Mwezi Agosti takriban watoto 160 walifariki katika hospitali ya Gorakhpur Polisi nchini India wanachunguza vifo vya watoto kadhaa wanaozaliwa kwenye hospitali ya Farrukhabad, huko Pradesh. Watoto 49 walifariki katika hospitali ya Ram Manohar Lohia ndani ya mwezi mmoja wakiwemo 30 waliofariki kutokana na tatizo linalojulikana kama "perinatal asphyxia". Hali hiyo inasababishwa na viwango vya chini vya hewa wakati wa kuzaliwa. Mwezi Agosti takriban watoto 160 walifariki katika hospitali ya Gorakhpur katika jimbo hilo hilo. Baadhi ya vifo vilitajwa kusababishwa na ukosefu ya hewa. Image caption Farrukhabad na Gorakhpur Lakini mafisa wa vyeo vya juu serikalini wamekana kuwa hiyo ndiyo sababu kutokea vifo kwenye hospitali zote. Kwenye uchunguzi wa hivi majuzi ripoti ya serikali iliwalaumu madaktari kwa vifo vya watoto 30, na kusababisha kufanywa uchunguzi Vivo vyote 49 vilitokea kati ya Julai 21 na Agosti 20. Poisli ...

Uchaguzi mpya wa urais Kenya kufanyika Oktoba 17

Image
Haki miliki ya picha AFP/GETY Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya imetangaza kwamba uchaguzi mpya wa urais nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba. Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema uchaguzi huo utashirikisha wagombea wawili pekee wa urais, Rais Uhuru Kenyatta na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. "Hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wa urais katika uchaguzi huo upya. Waliopinga matokeo ya uchaguzi kortini, Bw Raila Odinga na mgombea mwenza wake Stephen Kalonzo Musyoka na mshtakiwa wa tatu Rais Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Samoei Ruto, watakuwa ndio wagombea pekee," taarifa ya bw Chebukati imesema. Katika kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, Mahakama ya Juu iliiwekea lawama Tume ya Uchaguzi. Majaji wa tume hiyo hawakuandaa uchanguzi huo kwa viwango vilivyowekwa kwenye katiba na sheria za uchaguzi, na kwamba kulitokea kasoro nyingi sana katika mchakato wa kupeperusha matokeo. Haki miliki ya pic...

Visiwa vya Caribbean vyajiandaa kwa kimbunga kikali

Image
Image caption Hurricane Irma kinatajwa kuwa kitasababisha madhara makubwa kama ilivyokuwa kwa Hurricane Harvey Gavana wa Florida ametangaza hali ya hatari baada ya kimbunga Irma kuonekana kujiimarisha zaidi. Irma kinaonekana kuelekea pande za Mashariki mwa visiwa vya Caribbean na kinatarajiwa kuingia Florida siku ya Jumatano. Kinatarajiwa kupiga sehemu kadhaa za visiwa vya Caribbean vikiwemo Leewards, Haiti na kisiwa cha Marekani cha Puerto Rico, kabla ya kuelekea Florida. Irma kimepata nguvu na upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita 215 kwa saa, na kinatarajiwa kupata nguvu zaidi ndani ya saa 48 zinazokuja. Kimbunga hicho kinakuja wakati wenyeji wa majimbo ya Texas na Louisiana wakikadiria athari za kimbunga Harvey, ambacho kilisababisha mvua kubwa na kuharibu maefu ya nyumba. Hata hivyo kituo cha vimbunga cha Marekani kinasema kuwa ni mapema sana kutabiri njia kitapitia Irma au athari zake kwa Marekani. Image caption Wakazi wa Puerto Rico wakiondoa baadhi ya vitu mu...

Marekani yailaumu Korea Kaskazini kwa kuomba vita

Image
Image caption Haley amesema teknolojia ya Korea ya Kaskazini kwenye mabomu ya nyukilia ni ya hatari na haina mfano Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa ameilaumu Korea ya Kaskazini kwa kulazimisha vita kutokana na majaribio yake ya makombora ya mara kwa mara. Nikki Haley ametaka kuwepo kwa muda wa dharura wa Baraza la Umoja wa Mataifa utakao jibu majaribio hayo kwa hatua kali. "Vita sio kitu ambacho Marekani ingetaka," alisema. "Hatutaki vita kwa sasa lakini uvumilivu wa nchi yetu hautuzuii." Baadae, kupitia mazungumzo ya simu na Rais Trump, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema atahimiza kuwepo kwa vikwazo vikali kutoka umoja wa nchi za ulaya dhidi ya Pyongyang. Hata hivyo, China imesisitiza wito wake wa kutaka pande zote zirudi katika meza ya mazungumzo. Image caption Baraza la usalama la umoja wa mataifa mara ya mwisho liliweka vikwazo kwa Korea Kaskazini juu ya bidhaa zake mwezi Agosti Ripoti zinasema kuwa Korea Kaskazini inajiandaa...