Posts
Showing posts from December 11, 2017
Man United yalala 2-1 kwa Man City
- Get link
- X
- Other Apps
Image caption City haijafungwa mchezo wowote kwenye ligi msimu huu Manchester City imeendeleza ubabe wake kwenye ligi kuu soka ya England baada ya kumchapa hasimu wake wa jiji moja Manchester United 2-1. Katika mchezo huo ambao City ilimiliki mpira wakati mwingi, ilipata goli lake la kwanza kupitia David Silva dakika ya 43 kabla ya Marcus Rashford kusawazisha dakika ya 45 na Nicolás Otamendi kupachika la pili na la ushindi dakika ya 54. Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kwa sasa ni wazi asilimia kuwa ya ubingwa msimu huu ikaenda kwa City. Image caption Nusura Lukaku asawazishe matokeo dakika za mwisho wa mchezo kabla ya mlinda mlango wa City Ederson kuokoa ''Wamecheza vizuri, wengi walitarajia hili, ni vigumu kuwakabili kama hauna timu imara zaidi yao, tumemkosa Pogba ambaye angeweza kuleta madhara kwao, nafikiri wanaweza kuwa mabingwa msimu huu,'' alisema Mourinho. Meneja wa City Pep Guardiola ameisifu timu yake kwa kucheza kama Barcelon...
Shughuli z kumuapisha Odinga kama Rais wa Kenya zaahirishwa
- Get link
- X
- Other Apps
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Raila Odinga Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya NASA, umetangaza kuahirishwa kwa shughuli ya kumuapisha kinara mkuu wa muungano huo Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama rais na makamu wa rais mtawalia wa Jamhuri ya Kenya. Shughuli hiyo ilikuwa imepangiwa kuandaliwa Jumanne tarehe 12 mwezi huu. Katika taarifa iliyotolewa leo na muungano wa NASA ni kuwa tarehe mpya ya kuapishwa kwa Bw. Odinga na Musyoka, na pia kuzinduliwa kwa mabunge ya wananchi itatangazwa baadaye. Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi mkuu ambao ulifanyika tarehe 26 mwezi Oktoba ambapo Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi. Uchaguzi huo wa tarehe 26 ulikuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu. Wakati wa kuapishwa kwake tarehe 28 mwezi uliopita, Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kuunganisha taifa katika muhula wake wa pili uongozini katika sherehe ambayo ilisu...
Moto wa nyika watishia mji wa Santa Barbara California
- Get link
- X
- Other Apps
Haki miliki ya picha SANTA BARBARA COUNTY FD Image caption Moto wa nyika California watishia mji wa Santa Barbara Shughuli mpya ya kuhamisha watu umeamrishwa baada ya moto mkubwa wa nyika kusini mwa jimbo la California kukosa kudhibitiwa siku ya Jumapili. Ukichochewa na upepo moto huo wa nyika wa Thomas, unatishia mji wa pwani wa Santa Barbara na mwingine ulio karibu wa Carpinteria. Wazima moto mapema walisema kwa kuwa moto huo ulikuwa unadhibitiwa lakini wakaongeza kuwa umeteketeza eneo lenye ukubwa wa jimbo la Chicago. Licha ya moto mwingine katika jimbo hilo kudhibitiwa kwa sehemu kubwa, moto wa Thomas umedhibitiwa kwa asilimia 15 tu. Amri ya kuhama imetowa usiku sehemu za Carpinteria karibu na msitu wa Los Padres kilomita 160 kutoka Los Angeles. Haki miliki ya picha NASA/EPA Image caption Satellite imagery shows the vast Thomas Fire, north of Los Angeles, which has spread as far as the Pacific coast Watabiri walisema kuwa upepo unatarajiwa kuongezeka siku ya leo k...
Netanyahu: Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka 3000
- Get link
- X
- Other Apps
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Netanyahu: Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka 3000 Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa wapalestina ni lazima wakubali kuwa Jurusalem ndio mji mkuu wa Israel ili amani iweze kupatikana. Netanyahu alisema Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka 3,000 na haujakuwa mji mku wa watu wengine. Aliongea huku maandamano yakiendelea kwenye ulimwengu wa kiislamu kufuatia hatua ya Marekani kuutambua Jurusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Ghasia zilizuka karibu na ubalozi wa Marekani nchini Lebanon na kwingineno siku ya Jumapili. Jerusalem kwenyewe, mpalestina mmoja alikamatwa kwa kumdunga kisu na kumjeruhiwa vibaya afisa wa usalama wa Israel karibu na kituo kimoja cha basi. Akiongea mjini Paris baada ya mazungumzo na rais wa Ufaransa Emmauel Macron, Bw Netanyahu alisema kuwa jitihada za kuwanyima wayahudi mji wa wa Jerusalem ni kitu kibaya. "Unaweza kusoma katika kitabu kizuri zaidi, kinaitwa Biblia...
Papa Francis, Guterres watoa maoni uamuzi wa Trump juu ya Israel
- Get link
- X
- Other Apps
Image caption Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema hatua ya rais Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel inaleta wasi wasi katika jitihada za kuleta amani katika mzozo wa Israel na Palestina. Akizungumza na CNN Guterres ametoa msimamo huo siku ambayo pia msemaji wa makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ameishutumu serikali ya Palestina. Msemaji huyo ameongeza hakufurahiswa na kitendo cha rais wa Palestina Mahmoud Abbas kushindwa kukutana na kiongozi huyo wa Marekani kwa sababu ya mzozo wa mji wa Jerusalem. Waandamanaji wameendelea kukusanyika mitaani katika nchi za Kiaarabu wakipinga hatua hiyo ya raia Trump. Image caption Papa Francis,asema Israel ni ya Wakristo,Wayahud na Waislam. Naye Papa Francis ambaye ni kiongozi wa kidini wa wakatoliki wapatao billion moja duniani ametoa maoni yake,akisema kuwa Jerusalem ni mji mtakatifu kwa wakristo,Wayahudi na Waislam. Amesema ni mazungum...