Tottenham yaichapa Nicosia bao 3-0
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Totten ham yaichapa Nicosia bao 3-0-Uefa Michuano ya klabu bingwa Ulaya (Uefa Champions League) hatua ya makundi imepigwa usiku wa kuamkia leo jumatano kwa mechi kadhaa hatua ya Makundi. Katika mechi za Kundi E - Sevila wamechomoza na ushindi wa 3-0 dhidi ya Maribor, Spartak Moscow wametoshana nguvu na Liverpool kwa sare ya bao 1-1, Kundi F- Manchester City wameshinda dhidi ya Shakatar Donestsk bao 2-0 . Sc Napoli imeshinda bao 3-1 baina ya Feyenoord, Kundi G- Besiktas imeshinda bao 2-0 dhidi ya Rasen Ball sports, Monaco imechapwa 3-0 na Fc Porto, Apoel Nicosia imechapwa bao 3-0 na Tottenham Hotspur, na Borussia Dortmund imefungwa na Real Madrid bao 3-1. Michuano hiyo inaendelea tena hii leo jumatano ambapo kundi A - Basel inaikabili Benfica, CSKA Moscow dhidi ya Manchester United, Kundi B- Anderlecht wanacheza na Celtic, PSG dhidi ya Bayern Munich, Kundi C - Qarabag dhidi ya As Roma , Atletico Madrid ni wenyeji wa Chelsea. K...