AJALI YA LORI LA MAFUTA DAR YASABABISHA KUTEKETEA KWA MALI NYINGI ZA WATU NA WENGINE KUPOTEZA MAISHA. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema wakimsikiliza miliki wa Nyumba ya kulala wageni United State na bar, Laurent Kasiga iliyopo Mbagala Rangi tatu, Dar es Salaam ambayo iliteketea kwa moto uliotokana na roli la mafuta lililopinduka na kuwaka moto wakati vijana wakiiba mafuta. Mkuu wa Moa akikagua Nyumba hiyo ya kulala wageni iliyokuwa na vyumba 32 na sehemu ya vinywaji.(bar). Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiangalia mabaki ya tenki la lori la mauta lililosababisha moto huo. Lori hilo lilivyoteketea kwa moto uliosababishwa na moja kati ya wananchi waliokuwa wakichukua mafuta ambaye alifaliki baada ya moto huo kumzingila. Moja kati ya duka la vifaa vya pikipiki lililo teketea kwa moto. Wahanga wa jana hili la moto waliokuwa wakifanya biashara ya...
Posts
Showing posts from October 14, 2014
- Get link
- X
- Other Apps
KUMBUKUMBU YA MIAKA 15 TANGU KIFO CHA MWALIMU NYERERE Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. WATANZANIA leo tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 tangu kufariki kwa muasisi na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, 1999 akiwa nchini Uingereza alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa ya damu. Akizindua rasmi maadhimisho ya kumbukumbu hizo jana, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Kate Kamba alisema kitaifa maadhimisho hayo yatafanyika mkoani Tabora.