Watu 235 wauawa katika shambulio la msikiti Misri
Haki miliki ya picha EPA Image caption Wanamgambo waliulenga msikiti mmoja karibu na eneo la al-Arish Wanamgambo wametekeleza shambulio la bomu na ufyatuaji wa risasi katika msikiti mmoja uliopo kaskazini mwa eneo la Sinai na kuwaua takriban watu 235 kulingana na chombo cha habari cha taifa. Walioshuhudia wanasema kuwa msikiti wa al-Rawda katika mji wa Bir al-Abeid , karibu na al-Arish ulilengwa wakati wa ibada ya Ijumaa. Maafisa wa polisi wanasema kuwa wanaume wanne waliokuwa ndani ya gari moja waliwafyatulia risasi waliokuwa wakiabudu kulingana na chombo cha habari cha AP. Misri imekuwa ikikabiliana na wanamgambo katika eneo hilo tangu 2013. Kumekuwa na mshambulio ya mara kwa mara yanayolaumiwa kutekelezwa na wanamgambo katika rasi ya Sinai lakini hilo ni shambulio baya zaidi kuwahi kufanyika. Picha katika eneo la mkasa huo zinaonyesha damu iliomwagika ndani ya msikiti. Image caption Ramani ya eneo la al-Arish Takriba watu 125 walijeruhiwa ripoti zinasema. Ripo...