WASIOJULIKANA WAUA WANAUME WAWILI WALIOLALA CHUMBA KIMOJA GESTI JIJINI TANGA
UTATA umeibuka baada ya miili ya watu wawili waliouawa na watu wasiojulikana kukutwa katika nyumba ya kulala wageni mjini Tanga ikiwa haina nguo na imefungwa kamba za miguu na mikononi. Katika tukio hilo ambalo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedicto Wakulyamba miili ya watu wawili, wote wanaume, iligunduliwa jana majira ya saa mbili asubuhi na mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ya Bomai Inn iliyopo Kata ya Majengo jijini Tanga. Kamanda Wakulyamba aliwaambia waandishi wa habari jijini Tanga jana kuwa mhudumu wa nyumba hiyo ambaye hakumtaja kwa jina, alibaini kuwapo kwa miili hiyo alipotaka kufanya usafi ndani ya chumba hicho. "Majira ya saa mbili asubuhi wakati mhudumu alipoingia ndani ya chumba hicho namba 303 kwa ajili ya kufanya usafi, alikutana na miili ya watu hao wawili wote ni wanaume ikiwa imelala chini, imefungwa kamba miguuni na mikononi," alisema. Kamanda huyo alisema miili hiyo ni ya watu wanaokadiriwa kuwa na umri...