Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria aendelea kupata nafuu
Image caption Rais wa Nigeria Bw Muhammadu Buhari Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ambaye anatibiwa jijini London kwa ugonjwa ambao bado haujatajwa, amezima kimya kirefu na kuzungumza. Kwa njia ya taarifa, Bwana Buhari amesema kuwa "matibabu yanendelea vyema, huku afya yake ikiimarika pakubwa". Hata hivyo, Rais ameongeza kusema kuwa, hata ingawa anajihisi kurejea nyumbani, madakatari bado wakimhudumia, huku akisema sasa ameanza kuzoea kufuata amri na maagizo badala ya kutoa amri. Kimya chake cha muda mrefu, kimezua malumbano kuwa, anafaa arejee Nigeria ama ajiuzulu kiti cha Urais. Tetesi kuhusiana na afya ya Bwana Buhari, imedumu kwa muda mrefu, tangu alipokwenda jijini London kwa matibabu, mwezi Juni mwaka jana. Makamu wa Rais Yemi Osinbajo, amekuwa akitawala Nigeria muda huu wote Buhari akiendelea na matibu.