Robinho: Mshambuliaji wa Brazil ahukumiwa kwenda jela kwa ubakaji
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Robinho aliifungia Brazil mabao 28 katika michezo 100 Mchezaji soka wa Brazil Robinho amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela kwa kushiriki katika genge lililombaka mwanamke mmoja mjini Milan mwaka 2013. Mahakma ya Italia imesema kuwa Robinho mwenye umri wa miaka 33- na raia wengine wa Brazil walimbaka mwanamke raia wa Albania , aliekuwa na umri wa miaka 22, baada ya kumnwesha pombe kwenye kilabu cha usiku mjini Milan. Mchezaji huyo wa safu ya ushambuliaji, aliyeondoka katika klabu ya AC Milan mnamo mwaka 2015 baada ya kuichezea miaka mitano hakuwepo mahakamani wakati wa hukumu hiyo lakini alikana mashataka dhidi yake kupitia wakili wake. Hukumu hiyo haitatolewa hadi pale mchakato wa rufaa utakapokamilika. Robinho, aliichezea Manchester City na sasa anachezea timu ya Atletico Mineiro nchini Brazil. Ujumbe kwenye ukurasa wa Instagram wa Robinho unasema "tayari amekwisha jitetea dhidi ya shutuma, akisisitiza kuwa hakus...