Posts

Showing posts from July 23, 2015

Ajali Mbaya ya Basi la Simiyu Express Yaua Watu Wengi Dodoma Usiku wa Kuamkia Leo

Image
Ajali Mbaya ya Basi la Simiyu Express Yaua Watu Wengi Dodoma Usiku wa Kuamkia Leo Sos Mpekuzi blog Taarifa kutoka mkoani Dodoma zinasema watu  zaidi  ya 10  wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo , huku zaidi ya abiria 40 wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS walilokua wakisafiria kutoka Mwanza kwenda DSM kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga mbuyu na kisha kupinduka.   Taarifa zinasema ajali hiyo ni mbaya sana kuwahi kutokea mkoani Dodoma.Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu.

Ziara ya Obama:Anga ya Kenya kufungwa

Image
Ziara ya Obama:Anga ya Kenya kufungwa Ziara ya Obama nchini kenya Shirika linalosimamia safari za ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga ya Kenya itafungwa kwa muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii ili kuruhusu ndege ya rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi. Kwa mujibu wa shirika hilo, agizo hilo litatekelezwa katika viwanja vyote vya ndege nchini Kenya na kuwa anga hiyo itafunguliwa muda tu pale ndege hiyo ya rais Obama itakapokuwa imetua. Shirika hilo limesema kuwa limeyaandikia mashirika yote ya ndege na pia kampuni zote za usafiri kuhusiana na agizo hilo na kuwa safari za ndege kadhaa zitacheleweshwa siku hiyo na pia siku ya jumapili wakati rais Obama atakapokuwa akiondoka nchini Kenya kuelekea Ethiopia kwa muda wa dakika arubaini.   ...

Gereza la Guantanamo lakaribia kufungwa

Image
Gereza la Guantanamo lakaribia kufungwa gereza la Guantanamo linamilikiwa na Marekani Ikulu ya White house imesema kuwa mipango ya kulifunga gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba imefikia awamu za mwisho. Rais Barack Obama anasemekana kupatia kipa umbele suala la gereza hilo tangu aingie madarakani mwaka wa 2009 lakini limekumbwa na vizuizi kadhaa.   gereza lililo n aulinzi mkali la Guantanamo Gereza hilo la Guantanamo, ambalo limepewa jina la umaarufu kuwa Gitmo - limekuwa likitumiwa na Marekani kuwazuilia wapiganaji kutoka vita vya Iraq na vya Afghanistan bila kufunguliwa mashtaka yoyote. Rais Obama alitoa agizo la kirais kufungwa kwa kituo hicho mara moja katika siku yake ya kwanza. Lakini baraza la Congress lilikataa kuwahamisha wafungwa wa huko kuwaleta...