Posts

Showing posts from August 25, 2017

UN yataka mapigano kusitishwa Syria kupisha misaada

Image
Image caption Raia wengi wapo katika hali mbaya kwa kukosa chakula na huduma nyingine muhimu Umoja wa Mataifa umetoa wito kusimamishwa kwa muda mapigano katika mji wa Ragga nchini Syria, kuruhusu idadi ya raia waliopo katika eneo hilo la mapigano kuondoka. Mkuu wa misaada ya kibinadamu nchini Syria, Jan Egeland, anasema mji wa Raqqa yawezekana kwa sasa ni moja kati maeneo hatari duniani na kutaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kutoa mwanya kwa raia kutoroka katika eneo hilo. Amesema kuwa wapiganaji wa Islamic State wanatumia kundi la raia waliobaki kama kinga ya kivita. Hata hivyo idadi hiyo ya raia wapatao 25,000 kwa wamekwama ndani ya mji huo huku kukiwa na mfululizo wa mashambulizi ya anga kwa juma moja lililopita. Image caption Ragga unatajwa kuwa miongoni mwa miji hatari zaidi duniani Shirika la kimataifa la Amnesty linasema mamia ya watu wameuawa tangua mashambulizi hayo yalipoanza katika mji wa Raqqa mwezi june mwaka huu. Wapiganaji wa IS wanatuhumiwa na umoja...

Everton waingia hatua ya makundi Europa League

Image
Haki miliki ya picha Image caption Sigurdsson alifunga bao mechi yake ya kwanza aliyokuwa kwenye kikosi cha kuanza mechi Ulaya tangu Machi 2014. Gylfi Sigurdsson alianza mechi yake ya kwanza Everton kwa kufunga bao akiwa hatua 50 kutoka kwenye goli na kusaidia vijana hao wa Ronald Koeman kufika hatua ya makundi katika ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League. Everton walitoka sare ya 1-1 ugenini mechi hiyo dhidi ya Hajduk Split ya Croatia lakini wakasonga kwa ushindi wa jumla wa 3-1. Klabu hiyo ya England ilikuwa ikiongoza 2-0 kutoka kwa matokeo ya mechi ya kwanza na matumaini yao yalionekana kukaribia kufutika baada ya Josip Radosevic kumbwaga kipa Jordan Pickford. Lakini Sigurdsson, aliyekuwa akichezea Everton mara yake ya pili tangu wamnunue £45m kutoka Swansea alisawazisha sekunde 14 baada ya kuanza kwa kipindi cha pili. Bao la Sigurdsson liliwaacha Hajduk wakihitaji kufunga mabao matatu ndipo wafanikiwe kusonga. Wayne Rooney, aliyekuwa kwenye kikosi cha kuanza mec...

Yingluck: Mahakama yatoa kibali waziri mkuu wa zamani Thailand akamatwe

Image
Haki miliki ya pich Image caption Mamia ya wafuasi wa Bi Yingluck walifika nje ya majengo ya mahakama ya juu Bangkok Mahakama ya Juu nchini Thailand imeahirisha kikao cha kutoa hukumu katika kesi ambapo waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Yingluck Shinawatra ameshtakiwa makosa ya uhalifu ya kuzembea kazini. Majaji hao wakiwa mjini Bangkok wametoa kibali cha kukamatwa kwake wakisema hawaamini alivyosema kwamba amekosa kufika mahakamani kwa sababu anaugua. Mahakama imeahidi kutoa huku tarehe 27 Septemba. Ijumaa, mawakili wa Bi Yingluck waliomba hukumu icheleweshwe na kuambia mahakama kwamba anaugua ugonjwa wa vertigo na hawangeweza kufika kortini. Lakini taarifa rasmi ya Mahakama ya Juu imesema waendesha mashtaka "hawaamini mshtakiwa ni mgonjwa kwani hakuna cheti chochote cha matibabu kilichowasilishwa kwa mahakama, na kwamba hali yake ya afya si mbaya mno kiasi kwamba hawezi kufika kortini." Mahakama imesema itatoa kibali cha kukamatwa kwake kwani anaweza kuiki...

Taarifa muhimu kwa wote walioomba na watakaoomba kazi Serikalini

Image
Mtakumbuka Serikali katika mwaka wa fedha uliomalizika  2016/2017  iliahidi kutoa Ajira serikalini zaidi ya  52,000  kwa Watanzania, ambapo katika siku za hivi karibuni Serikali imekuwa ikitoa vibali vya kuajiriwa watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo Waalimu wa Sayansi, Kada za Afya na maeneo mengine kulingana na mahitaji. Kama mnavyofahamu mojawapo ya jukumu la msingi la kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni pamoja na kuendesha mchakato wa ajira kwa niaba ya waajiri mbalimbali na hatimae kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi wanaofaulu usaili, ambapo tangu Serikali ilipoanza kutoa vibali baada ya kusitishwa tumeshapokea jumla ya vibali kwa ajili ya mamlaka za Ajira  239,  kati ya hivyo vipo ambavyo vimeshafanyiwa kazi na vingine mchakato wake unaendelea katika hatua mbalimbali. Aidha, baadhi ya vibali ambavyo mchakato wake umeshakamilika ni pamoja na  kibali cha Mamlaka ya Chakula na Dawa  (TFDA) ...

DK. KIGWANGALLA AZINDUA ZOEZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI NA SHINGO YA KIKZAZI MKOANI RUVUMA

Image
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Hamisi Kigwangalla mapema jana Agosti 24,2017, amezindua rasmi zoezi la upimaji  wa Afya bure  kwa akina mama linalofanyika kwa siku tatu kwenye uwanja wa Majimaji  na maeneo mengine ya Songea  Mkoani Ruvuma.  Zoezi hilo linaratibiwa na Chama Cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kwa ushirikiano na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Serikali ya Mkoa wa Ruvuma. Kampeni itahusisha upimaji wa Saratani ya Matiti, Saratani ya Shingo ya Kizazi, Kisukari, Shinikizo la damu (Hypertension), Magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza na Ugonjwa mengine yakiwemo ya kuambukiza (Kifua Kikuu). Dk. Kigwangalla  aliwashukuru MEWATA, kwakuwezesha zoezi hilola upimaji Afya bure  ambapo zoezi hilo linaonyesha dhamira ya kuhakikisha kwamba jamii ya Kitanzania inahamasika katika kupunguza tatizo la saratani kwa ujumla, hususani saratani ya matiti na mlango wa kizazi n...

WAZIRI MWAKYEMBE AWAPA BARAKA WATOTO WA TANZANIA KWENDA MAN CITY KWA MAJARIBIO.

Image
Waziri wa michezo nchini Tanzania Mh.Dk Harrison Mwakyembe amewatakia safari njema watoto waliochaguliwa na kampuni ya Tecno mobile kwenda kufanya majaribio ya kucheza mpira wa miguu katika academy ya klabu ya Manchester City nchiniUingereza. Malimi Majaliwa wa kwanza kushoto na Daudi DAmasi wakiwa katika picha ya pamoja baada yakupewa Baraka za safari na Mh. Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe) Akiongea katika hafla hiyo fupi kutambulisha mbele ya waziri mpango huo, Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Tecno Mobile Bwana, Eric Mkomoya alisema kua kampuni ya Tecno Mobile ndio wadhamini pekee wa safari hiyo kupitia simu yao mpya Tecno Camon Cxto leo maalumu la machester city ambapo watoto hao wawili wataenda kupewa mafunzo yenye kiwango cha kimataifa lakin pia endapo watafanya vizuri wanaweza kuchaguliwa kuendelea kucheza katika klabu hiyo. ,(wadhamini wa kuuwa safari  (Wazazi na walezi wa vijana wanaokwenda Manchester city wakiwa katika picha ya...

NAIBU WAZIRI AAGIZA HALMASHAURI KUTAMBUA MAENEO YASIYOENDELEZWA NA YASIYOMIKILIWA KIHALALI

Image
Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali. Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea kuona Ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Maji Lamadi itakayosimamia mradi wa maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali . Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kutembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Bus...