Posts

Showing posts from December 1, 2017

MAGAZETI YA IJUMAA LEO DECEMBER MOSI,2017

Image

Gordon Reid atinga nusu fainali michuano ya Tennis Masters

Image
Image caption Gordon Reid anatarajiwa kupanda kwenye viwango vya kimataifa hivi karibuni Muingereza Gordon Reid ameshinda mchezo wake wa pili katika mashindano ya walemavu ya Tennis Masters na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuingia kwenye hatua ya nusu fainali itakayopigwa mjini Loughborough. Baada ya kupoteza mbele ya bingwa Joachim Gerard siku ya Jumatano, Reid amemshinda Nicolas Peifer wa Ufaranda kwa seti 3-6 6-4 6-3. Muingereza mwenzake Andy Lapthorne nae pia amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kumchapa Heath Davidson wa Australia kwa seti 6-2 7-5. Alfie Hewett naLucy Shuker walipoteza michezo yao. Hewett, namba mbili kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume, alipangwa kucheza na Shingo Kunieda wa Japan lakini alipoteza kwa seti 2-6 6-4 6-2 baada ya kuumia bega.

Sam Allardyce achukua mikoba kuinoa Everton

Image
Image caption Sam Allardyce (katikati) alionekana na mmiliki wa Everton Farhad Moshiri katika uwanja wa Goodison Park siku ya Jumatano Klabu ya soka ya Everton ya Uingereza imempa kibarua cha kuinoa klabu hiyo meneja Sam Allardyce. Allardyce amesema ana furaha na faraja kujiunga na klabu ya Everton. Big Sam mwenye miaka 63 kocha wa zamani wa timu ya taifa ya England amesaini mkataba utakaomuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2019 akichukua mikoba ya Ronald Koeman aliyetimuliwa mwezi Oktoba baada ya timu hiyo kuanza ligi vibaya. Allardyce amekuwa nje ya uwanja tokea alipoachana na klabu ya Crystal Palace mwezi Mei. Ni mashuhuri sana kwa kuzisaidia timu ambazo zinakaribia kushuka daraja zisailie kwenye EPL.

Tundu Lissu: Kushambuliwa kwangu kulichochewa na siasa Tanzania

Mwanasheria kuu wa chama upinzani Chadema nchini Tanzania Tundu Lissu, ambaye amekuwa akipokea matibabu Nairobi tangu alipopigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma mwezi Septemba, amesema anaamini kushambuliwa kwake kulihusiana na siasa nchini humo. Akizungumza na BBC, mbunge huyo wa Singida Mashariki amelilaumu Bunge la nchi hiyo akisema halijachukua hatua zozote kumsaidia tangu kulazwa kwake hospitalini. Makamu wa Rais wa Tanzania Bi Samia Suluhu alimtembelea hospitalini mapema wiki hii. Bw Lissu amesema anaendelea kupata nafuu vyema. Juhudi za BBC za kuwasiliana na msemaji wa Bunge la Tanzania kuhusu tuhuma za Bw Lissu hazijafua dafu. Amezungumza na mwandishi wa BBC John Nene.

Alipua vilipuzi mahakamani na kujiua pamoja na mshukiwa

Image
Haki miliki ya picha DP.NPU.GOV.UA Image caption Magurunedi hayo yalilipuliwa wakati wa kusikizwa kwa kesi ya mauaji Mwanamume mmoja amelipua maguruneti mawili katika mahakama moja mashariki mwa Ukraine , akijiua pamoja na mmoja wa washukiwa wa mauaji ,kulingana na maafisa wa polisi. Mlipuko huo ulitokea wakati wa kikao cha kusikizwa kwa kesi hiyo mjini Nikopol katika jimbo la Dnipropetrovsk. Mtu huyo ni baba ya mmoja wa waathiriwa waliouawa kulingana na maafisa wa polisi. Takriban watu tisa walijeruhiwa, ikiwemo washtakiwa wawili , walinzi wawili afisa mmoja wa mahakama na raia. Washtakiwa hao watatu wanatuhumiwa kuifyatulia risasi gari moja na kuwaua abiria wawili mnamo mwezi Februari 2016 akiwemo mwana wa mtu ambaye alilipua vilipuzi hivyo , kulingana na vyombo vya habari. Kulingana na ripoti za awali mtu mmoja alitoa maguruneti mawili na kuyalipua wakati wa kusikizwa kwa kesi ya mauaji kulingana na mtandao wa Ukrainska Pravda ambao ulimnukuu msemaji wa polisi Yaros...