Watu 20 wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wakamatwa Zanzibar
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi-Unguja linawashikilia watu 20, ambao ni wanawake(12) na wanaume(8) kwa tuhuma za kukutwa wakifundishana kufanya mapenzi ya jinsia moja. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharib, Hassan Nassir amesema watu hao wamekamatwa wakati wakipatiwa mafunzo ya namna ya kuzitambua haki zao yaliyokuwa yakitolewa na taasisi iliyotambulika kwa jina la Bridge Initiative. “Ni kweli tuliweza kuwakamata kwa sababu walikuwa wakishiriki katika mapenzi ya jinsia moja kitu ambacho ni kinyume na sheria kisiwani zanzibar na ni ukiukaji wa sheria za Tanzania”, alisema Hassan pia akaongeza kuwa polisi wataongeza doria zao dhidi ya makundi kama hayo. Mwezi michache iliopita Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed alitangaza vita kwa wanaojihushisha na biashara hiyo haramu na alipiga ‘stop’ taasisi zinazofadhiri watu hao.