Posts

Showing posts from November 22, 2017

Je Robert Mugabe ni nani?

Image
Image caption Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amejiuzulu Mwaka 1980, Bw Mugabe alishinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu  Mwaka 1982 aliushutumu upinzani kwa kujaribu kupindua serikali Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake  Mwaka 1987,alibadilisha katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake  Uchumi ulidororeka baada ya mwaka 2000… Wakati Mugabe aliagiza kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara ya uchumi Mfumuko wa bei ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi kudororeka Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai  Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Bw Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi Ndoa yake na Grace Mugabe ,anayemzidi kwa maika 40, yaweza kuwa iliyomponza Wengi walikasirishwa na Grace kuandaliwa kuwa mrithi wake. Jeshi limeone...

Rais Robert Mugabe amejiuzulu

Image
Image caption Rais Robert Mugabe amejiuzulu Spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu . Spika wa bunge Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani ya mamlaka kulingana na chombo cha habari cha Reuters. Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake. Haki miliki ya picha AFP/GETTY Image caption Nukuu ya rais Mugabe alipokuwa akijiuzulu Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya Jumatano. Haki miliki ya picha AFP Image caption Raia wa Zimbabwe wafurahia kujiuzulu kwa Mugabe Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani. Je,ni Kiongozi mkombozi ,mfisadi au mwonevu? Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiw...

KUTOKA KWENYE MAGAZETI YA HARDNEWS TANZANIA, JUMANNE NOVEMBA 21/ 2017 YAKIWA NA VICHWA VIKUU VYA HABARI

Image
 

MBUNGE WA VITI MAALUM NJOMBE AWASAIDIA WANAWAKE VYEREHANI 370

Image
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe Neema Mgaya ametoa msaada wa vyerehani 370 vyenye thamani zaidi ya Milioni 90 kwa wanawake mkoani humo ili wajikwamue kiuchumi huku akiunga mkono juhudi za Serikali inayohimiza uchumi wa viwanda. Akizungumza Mjini Makambako wakati wa hafla ya kukabidhi vyerehani hivyo kwa baadhi ya wanawake, Mgaya amesema amefikia uamuzi huo ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa taifa la uchumi wa kati kupitia viwanda. Akibainisha zaidi ameeleza juhudi za kumkomboa mwanamke wa mkoa wa Njombe ni jambo linalopiganiwa kwa miaka mingi hivyo vyerehani hivyo vitawafungulia njia kuweza kujikwamua kiuchumi. “Nimekuwa sina papara katika utendaji wangu, mwaka jana nilitoa msaada wa vitabu vya ziada kwa Shule za Sekondari Halmashauri ya Makambako, ambapo kwa mwaka huu nimeamua kuunga mkono juhudi za serikali upande wa viwanda kwa kuwasadia wanawake hawa vyerehani hivi 370,”  alisema Mgaya. Akifafanua amesema anatambu...

Ujenzi mradi wa Kinyerezi II wafikia asilimia 84

Image
Imeelezwa kuwa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha Umeme wa kiasi cha megawati 240 kwa kutumia Gesi Asilia katika mradi wa Kinyerezi II umefikia asilimia 84. Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Meneja Miradi ya Umeme ya Kinyerezi, Mhandisi Stephen Manda wakati akitoa taarifa ya miradi ya Kinyerezi I (MW 150), Kinyerezi I-Extension (MW 185) na Kinyerezi II (MW 240) kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu. Naibu Waziri Mgalu alifanya ziara katika mitambo hiyo lengo likiwa ni kupata taarifa na kukagua kazi iliyofanywa na Wataalam wa TANESCO ya kusafisha na kuunga Bomba kubwa la Gesi katika mitambo ya Kinyerezi I iliyofanyika Novemba 18 na 19 mwaka huu na hivyo kusababisha upungufu wa Umeme katika gridi ya Taifa. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli hiyo, Mhandisi Manda alieleza kuwa TANESCO walikamilisha zoezi hilo kwa ufanisi na ilipofika mchana wa Novemba 20, 2017 mitambo hiyo iliingiza megawati 115 katika Gridi ya Taifa na hivyo kuboresha hali ya upatikanaji wa Umeme....

CCM YATEUA WAGOMBEA SITA WA UENYEKITI WA WILAYA ZA KICHAMA

Image
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanya uteuzi wa majina ya wagombea wa uenyekiti wa wilaya sita za kichama. Wilaya hizo ni Moshi Mjini, Hai, Siha, Makete, Musoma Mjini na Musoma Vijijini. Taarifa kwa umma iliyotolewa na CCM jana Jumatatu Novemba 20,2017 imesema Kamati Kuu ya chama hicho kwa niaba ya Halmashauri Kuu imeteua majina ya wagombea katika wilaya ya Hai ambayo ni ya Abdulah Mriri, Magai Maganda na Justice Masawe. Kwa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro walioteuliwa ni Justice Mkita, Wilfred Mossi na Humfrey Nnko, huku Wilaya ya Moshi Mjini wateule ni Absalom Mwakyoma, Joseph Mtui, Faraji Swai na Alhaji Omar Amin Shamba. Taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole imesema kwa Wilaya ya Makete wateule ni Aida Chengula, Mwawite Njajilo na Onna Nkwama; Wilaya ya Musoma Mjini ni Robert Sylvester, Magiri Maregesi, Amina Nyamgambwa na Daud Misango. CCM imesema wateule wa Musoma Vijijini ni Gerald Kasonyi, K...

NAIBU WAZIRI HASUNGA AKABIDHI MSAADA WA MABATI KWA SHULE YA MSINGI ILIYOATHIRIKA NA KIMBUNGA MKOANI IRINGA

Image
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kijiji cha Ubwachana, Donatus Lihoha mabati 60 kwa ajili ya kuezeka vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Kipanga ambayo iliezuliwa na kimbunga hivi karibuni ikiwa ni kutambua mchango wa wananchi katika uhifadhi shirikishi wa Kituo cha Mali Kale cha Isimila jana Mkoani Iringa. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakitwanga Kinu wakati wa ziara yake katika Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa (Boma) jana Mkoani humo. Katika jiihada za Serikali za kuendeleza ushirikiano na jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi nchini, Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa msaada wa mabati sitini kwa ajili ya kuezeka madarasa ya shule ya msingi Kipanga baada ya kuezuliwa na kimbunga hivi karibuni katika kijiji cha Ubwachana Wilaya ya Iringa mkoani Iringa. Msaada huo umetolewa jana na Naibu Waziri wa Mali...