Posts

Showing posts from December 4, 2017

Tetesi za Soka Ulaya.Jumatatu 4 .12 .2017

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Danny Rose Tottenham watamuuza mlinzi wa England Danny Rose, 27, kwenda Manchester United mwezi Januari lakini ikiwa watapewa kitita cha pauni milioni 45. (Daily Star Sunday) Meneja mpya wa Everton Sam Allardyce anapanga kumununua mchezaji wa safu ya kati wa Sevilla na Ufaransa Steven N'Zonzi, 27. (Mail on Sunday) Manchester United hawana mpango wa kulipa pauni miloni 100 kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 28 na badala yake wameweka thamani mchezaji huyo kuwa kati ya paunia milioni 50 na 60. (Sunday Mirror)  Haki miliki ya picha REX FEATURES Image caption Gareth Bale Chlesea wanasema afadhali wamuachilia kipa raia wa Ubelgijia Thibaut Courtois, 25, aondoke wakati mktaba wake utakamilika mwishoni mwa msimu mwaka 2019 badala ya kumuuza kwa Real Madrid mwisho wa msimu huu.  Manchaster Unites hawajakufa moto wa kumsaini mlinzi na West Brom na Northern Ireland Jonny Evans, 29, baada ya majaribio...

Mnangagwa alifanyia mabadiliko ya haraka baraza la mawaziri

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Mnangagwa alifanyia mabadiliko ya haraka baraza la mawaziri Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amefanyia baraza lake la mawaziri mabadiliko siku mbili baada ya kulitangaza baraza jipya Wakosoaji wanasema kuwa orodha ya kwanza ilionyesha kuwa mnangagwa hakuwa na mpango wa kuleta mabadiliko nchini humo. Wizara za elimu na kazi sasa zimefanyiwa mabadiliko ili kuambatana na katiba. Lakini makamanda wa jeshi ndo walipewa wizara za mashauri ya nchi za kigeni na ardhi. Siku 10 zilizopita alirudi kutoka uhamishoni kufuatia mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Robert Mugabe na kuahidi kuhudumia raia wote kwa njia sawa. Siku ya Jumamosoi serikali ilitangaza kuwa wizara mbili zemefanyiwa mabadiliko kuhakikisha kuwa katiba imefuatwa kwa misingi na jinsia, kikanda na mahitaji maalumu. Ripoti zinasema kuwa orodha kwanza hakufuata katiba ambayo inataka kuwepo mawaziri wasiokuwa wabunge. Baadhi ya wafuasi wa upinzani walisherehekea hatua ya kumuona...

Marekani mbioni kukabiliana na tishio la Korea Kaskazini

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption HR McMaster anasema hakuna muda uliobaki kutatua tatizo lililopo Mshauri wa masuala ya usalama wa Ikulu ya White House nchini Marekani, HR McMaster, amesema kuwa Marekani iko mbioni kukabiliana na tishio kutoka Korea Kaskazini Uwezekano wa kutokea vita unaongezeka kila siku lakini vita sio suluhu pekee, aliuambia mkutano wa ulinzi. Matamshi yake yanakuja siku tatu bqada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio lake la kwanza la kombora la masafa marefu katika miezi miwili kinyume na vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Kombora hilo lilipaa mbali na makombora mengine ambayo yalijaribiwa awali kbala ya kuanguka katika bahari ya Japan. Haki miliki ya picha KCNA Image caption Kombora la Hwasong-15 lilipaa mbali zaidi na makomboa mengine ya awali HR McMaster ameitaka China kuiwekea vikwazo vya mafuta taifa hilo ili kufanya kuwa vigumu kwa Pyongyang kujaza mafuta makombora yanayofanyiwa majaribio. Korea Kaskazini imeishutumu Marekani kwa kuchoc...

Mbunge mwanamume amposa mpenzi wa kiume bungeni Australia

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Tim Wilson Mbunge mwanamume nchini Australia ameposa kwa mpenzi wake wa kiume wakati wa kikao cha bunge cha kujadili kuhalalishwa ndoa za jinsia moja. Tim Wilson alimchumbia Ryan Bolger ambaye alikuwa ameketi eneo la umma. Wawili hao wamekuwa wapenzi kwa miaka 9. Mswada huo wa kuhalalisha ndoa ya jinsia moja uliwasilishwa bungeni siku ya Jumatatu baada ya kupitia bunge la Senate wiki iliyopita. "Katika hotuba yangu ya kwanza, ninatambua uhusiano wetu kwa pete iliyo kwenye mikono yetu yote ya kushoto. Pete hii ni jibu kwa maswalii ambayo hatutawezi kuyauliza," Bw Wilson alisema. "Kwa hivyo kuna kitu kimoja tu ambacho kimebaki kufanywa. Ryan Patrick Bolger utakubalia nikuoe ?" Swali hilo lilizua shangwe na pongezi, kaala ya Bw Bolger kujibu kwa sauti na kusema "ndiyo" Mapema Bw. Wilsni alizungumzia maisha yake ya kukua kama kijana mpenzi wa jinsia moja na kukumbana na unyanyapaa . Bw Wilson ni m...

Jordan yaionya Marekani ikiitaka isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Jordan yaitaka Marekani isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel Ayman Safadi alisema alimuambia waziri wa mashauri wa nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson kuwa hatua kama hiyo inaweza kuzua ghadhabu kubwa kwa nchi za kiarabu na ulimwengu wa kiisalmu. Kuna uvumi kuwa Rais Donald Trump atatangaza hilo hivi karibuni na kutimiza ahadi yake aliyotoa wakati wa kampeni. Jared Kushner, mkwe wa Trump alisema kuwa bado hakuna uamuzi uliofanywa. Katika mtandao wa Twitter, Bw Safadi alisema: #Nilizungumza na waziri Rex Tillerson kuhusu hatari ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Hatua kama hiyo inaweza kusababisha ghadhabu kwenye nchi za kiarabu na kwa ulimwengi wa kiislamu na kuzua misukosuko na pia kuhujumu jitihada za amani." Haki miliki ya picha AFP Image caption Kuna uvumi kuwa Rais Donald Trump atatangaza hilo hivi karibuni na kutimiza ahadi yake aliyotoa wakati wa kampeni. Hakuna jibu lolote kutoka kwa wizar...