Homa ya nguruwe yawaua watu 1,000 nchini India
Haki miliki ya picha Image caption Vifo vilivyotokana na homa ya nguruwe vimeongezeka sana mwaka huu India inaonekana kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nguruwe baada ya watu 1,094 kuthibitishwa kufariki kutokana na ugonjwa huo katika kipindi cha miezi minane iliyopita, taarifa rasmi ya serikali imesema. Katika wiki tatu zilizopita, idadi ya vifo imekuwa juu sana, ambapo watu 342 wamefariki. Jumla ya visa 22,186 vya maambukizi ya ugonjwa huo vimeripotiwa nchini humo. Idadi ya watu waliofariki mwaka huu ni mara nne zaidi ya idadi iliyoripotiwa katika kipindi sawa na hicho mwaka 2016 ambapo visa vya ugonjwa huo vilikuwa vimeshuka sana. Jimbo la Maharashtra magharibi mwa nchi hiyo ndilo lililoathirika zaidi ambapo waliofarikini ni 437 kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya. Jimbo hilo linafuatwa na jimbo jirani la Gujarat lililoshuhudia vifo 297. India ilikabiliwa na mlipuko mbaya wa homa hiyo miaka miwili iliyopita ambapo zaidi ya watu 1,900 walifariki. Lak...