Posts

Showing posts from September 10, 2017

“Ukibisha kapambane na kulipa mishahara wachezaji wako”-Haji Manara

Image
Mkuu wa  idara  ya habari na mawasiliano wa club ya Simba Haji Manara ni moja kati ya viongozi na wapenzi wa soka wanaojiamini sana na mara nyingi amekuwa akipenda kuandika post za utani kwa wapinzani wao Yanga. Haji Manara usiku huu kutoka katika instagram account yae ameandika ujumbe akiwa kapost picha ya kikosi  cha Simba kuwa kwa sasa Simba ndio Brand maarufu zaidi nchini kuliko zote, unaweza andika comment yako hapo chini.

Ally kiba kawajibu mnaosema kaiba wimbo wa ‘SEDUCE ME’

Image
Usiku wa September 9, 2017 Fiesta ilifanyika kwa mara ya kwanza jijini Arusha ambapo wasanii mbalimbali walitumbuiza kwenye stage na miongoni mwao ni msanii anayefanya muziki wa bongofleva Alikiba ambaye alipata nafasi ya kuzungumza na kituo cha Ayo Tv na kuelezea kuhusu kudaiwa kuiba wimbo wa   ‘Seduce me’ . Alikiba amesema kuwa sikweli kuhusu kudaiwa kuiba wimbo huo bali ni wimbo wake na hana tabia za kuchukua wimbo wa mtu japo amedai wimbo wake kwa sasa unafanya vizuri kwa kuwa ni mzuri. Bonyeza  PLAY  hapa chini kumsikia  Alikiba  akizungumza kila kitu chanzo AYO TV

Wapiganaji wa Rohingya watangaza kusitisha mapigano, Myanmar

Image
Haki miliki ya picha EPA Image caption Wa Rohingya wanaishutumu jeshi la Myanmar kwa kuteketeza vijiji vyao - Lakini utawala nchini Myanmar, unasema wanajeshi wake wanakabiliana na "magaidi" Katika taarifa nyingine Asubuhi hii ya leo, waasi wa kiislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar wametangaza upande mmoja makubaliano ya kusitisha mapigano leo Jumapili, ili kujaribu kupunguza mgogoro wa kibinadamu magharibi mwa taifa hilo. Mashambulio dhidi ya jeshi la taifa hilo yanayotekelezwa wapiganaji wa Arakan Rohingya Salvation Army, yalisababisha mapigano makali ya wiki mbili, ambapo zaidi ya watu laki tatu wa jamii ndogo ya Warohingya wamekimbilia nchi jirani la Bangladesh.  Image caption Ramani ya Myanmar Kundi hilo la waasi, yameiomba jeshi la nchi hiyo pia kuitisha wito wa kusitisha mapigano, huku likiomba mashirika ya utoaaji misaada ya kibinadamu kurejelea kazi zao za kusambaza misaada. Waziri mmoja wa serikali ya Myanmar ameiambia BBC kuwa, wengi wa Wa-Rohi...

Kimbunga Irma chakaribia Florida

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Upepo mkali wa kimbunga Irma kimeanza kushuhudiwa Florida Nguvu ya upepo mkali unaondamana na kimbunga, kimeanza kugonga visiwa kadhaa kusini mwa jimbo la Florida nchini Marekani, huku kimbunga kikiacha uharibifu mkubwa katika visiwa vilivyoko kwenye bahari ya Atlantic huko Caribbean, kuelekea Marekani. Kimbunga Irma, kinatarajiwa kugonga maeneo hayo, baadaye leo Jumapili. Viwango vya maji tayari vimeanza kuogezeka katika maeneo ya pwani ya Florida, eneo ambalo linatarajia kimbunga kikubwa kuwasili. Taharuki na hatma ya baadaye ya mji wa Tampa, ambao unakabiliana ana kwa ana na njia inakopitia kimbunga hicho, haijulikani. Image caption Ramani ya mwendo wa Kimbunga Irma Tampa inasemekana kuwa ni mji ulioko katika mazingira magumu zaidi nchini Marekani, hasa kuhusiana na hatari ya kugongwa mara kwa mara na vimbunga. Zaidi ya watu milioni 6 huko Florida wanaondolewa majumbani mwao- robo tatu ya idadi nzima ya watu wa jimbo ...