Posts

Showing posts from August 27, 2017

Mafuriko mabaya yatokea Marekani baada ya janga la kimbunga Harvey

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Rockport ni mojawepo ya maeneo yaliyoathirika vibaya na kimbunga hicho Gavana wa jimbo la Texas, Greg Abbott, anasema kuwa, mafuriko ya kutisha ndio swala lake kuu la msingi, huku mvua kubwa inayoandamana na kimbunga kiitwacho Harvey, ikiendelea kutatiza mambo katika jimbo hilo. Bwana Abbott anasema kwamba, miji miwili katika barabara inakopitia kimbunga hicho, Houston na Corpus Christi, tayari imepokea mvua zaidi ya Sentimita 50 na kiwango kinatarajiwa kuongezeka kwa mita moja zaidi, kabla ya kimbunga hicho kupungua, ifikiapo katikati ya wiki hii. Haki miliki ya picha AFP Image caption Mji wa Rockport haujasambaratishwa kabisa na kimbunga hicho, lakini uko katika hali mbaya Zaidi ya wafungwa 4,500 katika gereza moja kusini mwa Houston wamehamishiwa hadi gereza lingine mashariki mwa Texas kwa sababu ya kuongezeka kwa maji ya mto Brazos ulioko karibu. Maafisa wakuu wa jimbo hilo wamesema. Juhudi za uokoaji, zinatatizwa na upepo mkali....

Floyd Mayweather amembandua Conor McGregor katika ndondi, Las Vegas, Nevada

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Bondia Floyd Mayweather Jnr, akimlemea Conor McGregor kwa makonde mazito mazito kabla ya kumalizika raundi ya 10 Mchuano mkali wa ndondi kati ya Conor McGregor na mwanandondi Floyd Mayweather Jnr umemalizika huko Las Vegas, Nevada nchini Marekani, baada ya kuchelewa kuanza kwa muda wa saa moja hivi. Floyd Mayweather Jnr ameibuka mshindi katika mchuano huo. Maelfu ya watu wamefika katika mji wa Las Vegas katika jimbo la Nevada nchini Marekani, kutizama mchuano huo mkali wa ndondi, unaofanyika leo Jumapili. Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Floyd Mayweather mara tu baada ya kushinda Masumbwi hayo yalikuwa ya raundi kumi. Awali wachanganuzi walisema kuwa Floyd Mayweather Jnr alikuwa ameanza kulemewa katika raundi tatu za mwanzo na mpinzani wake, kabla ya kujizoazoa na kuanza kumrushia makonde mazito mazito Conor McGregor, ambaye alionekana kulemewa hasa kuanzia raundi ya saba. Alishindwa kuhimili makonde mazito ya Ma...

Floyd Maywether amezima tambo za McGregor kwa TKO

Image
Baada ya headlines za tambo za bondia  Conor McGregor  kuelekea pambano dhidi ya  Floyd Maywether   ambaye hajawahi kupoteza pambano, asubuhi ya August 27 katika ukumbi wa   T-Mobile Arena  mjini  Nevada, USA  majibu yalipatikana. Mayweather  alikuwa anaingia kucheza pambano lake la 50 dhidi ya  McGregor  ambaye yeye lilikuwa ni pambano lake la 25 akiwa ndio kapoteza kwa mara ya pili na kashinda mara ya 23, ushindi wa leo wa Mayweather  unakuja baada ya kumpiga bondi wa  Philipino  Manny Pacquiao  May 3 2015 kwa point mjini  Las Vegas . Bondia  Floyd Mayweather  leo ameshinda pambano lake la 50 akiwa kacheza mapambano 50 bila kupoteza, amefanikiwa kuendelea kutetea rekodi yake kwa kumpiga  Conor McGregor  kwa  Technical Knock Out   (TKO) katika round ya 10 pambano la round 12. Video ya dakika 2 ikionyesha Hat-Trick ya Okwi iliyookoa Milioni ...