Posts

Showing posts from September 8, 2017

Mitandao 7 ya dunia iliyoripoti tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi

Image
Jana September 7, 2017 Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria wa CHADEMA  Tundu Lissu  alipigwa risasi na watu wasiojulikana baada ya kushambulia gari lake akiwa nyumbani muda mfupi baada ya kumaliza shughuli za Bunge Dodoma. Tukio hilo limegusa hisia za watu wengi huku vyombo mbalimbali vya habari vikiripoti tukio hilo kwa namna ya pekee ambapo katika kuhakikisha taarifa zinasambaa duniani kote mitandao mingi ya kimataifa imerusha habari hii wakiziandikia headlines mbalimbali lakini iliyoonesha kusikitishwa na tukio hilo. ALJAZEERA DAILY NATION REUTERS ABC NEWS NEW VISION JEUNE AFRIQUE FOX NEWS WORLD Maagizo ya Waziri Nchemba baada ya Lissu kupigwa risasi Polisi na RC Dodoma waongelea Tundu Lissu kupigwa risasi Na ayo tv

FIFA yataka mchezo kati ya Afrika Kusini na Senegal urudiwe

Image
Image caption Mwamuzi Joseph Lamptey kutoka Ghana amefungiwa maisha kujihusisha na soka Shirikisho la kandanda la Kimataifa FIFA, limeamuru mchezo kati ya Afrika Kusini na Senegal uliofanyika Novemba 12 urudiwe . Uamuzi huo umetolewa baada ya mwamuzi wa mchezo huo Joseph Lamptey kuvurunda kimaamuzi katika mchezo huo, hivyo ameadhibiwa na Kamati ya nidhamu ya FIFA . Image caption Mchezo huo uligubikwa na maamuzi kadhaa ya utata Mchezo huo utarudiwa Novemba 2017 katika kalenda ya kimataifa, kwenye tarehe ambayo itatajwa. Bafana Bafana waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba wa Teranga katika mchezo huo.

Watu nchini Australia wasalimisha bunduki 26,000

Image
Haki miliki ya picha AUSTRALIAN GOVERNMENT Image caption Watu nchini Australia wasalimisha bunduki 26,000 Watu nchini Australia wamesalismisha karibu bunduki 26,000 kwenye mpango wa kwaza wa kutoa msahama wa walio na bundukia zisizo na vibali tangu watu wengi wapigwe risasi mwaka 1996. Msamaha huo ulianza Julai mosi kusaidia kukabiliana na ugaidi uliokuwa ukikua na kuingia kwa silaha nchini humo. Ni haramu kumiliki bunduki isiyo na kibali nchini Australia. Wale ambao watapatwa nje ya msamaha huo watapigwa faini ya doa 225,000 na hadi kifungo cha miaka 14 jela Mpango huo wa sasa ambao unaendelea hadi Septemba 30, una maana kuwa watu nchini Australia wanaweza kusalimisha bunduki ambazo hazina vibali na vitu vingine kama hivvyo bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria. Waziri wa sheria Michael Keenan anasema kuwa matokeo mazuri hadi sasa yataifnya nchi kuwa salama. Polisi wanakadiria kuwa kuwa kuna hadi bunduki 260,000 haramu nchini Australia, zingine zikitumiwa kwa uhalif...

Kimbunga Irma chaendelea na uharibifu mkubwa huko Caribbean

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Irma kikionekana kutoka angani Kimbunga Irma kimeelekea visiwa vya Turks na Caicos baada ya kusababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean na kuwaua takriban watu 14. Visiwa vilivyo nyanda za chini vinaripotiwa kuwa kwenye hatari kubwa kukiwa na uwezekano wa kupigwa na mawimbi ya hadi urefu wa mita 6 kuliko viwango vya kawaida. Haki miliki ya picha AFP Image caption Mitaa iliyofurika huko St Martin Kumeripotiwa uharibifu na mafuriko nchini Haiti ambapo miundo mbinu bado ni mibaya tangu litokee tetemeo la ardhi mwaka 2010. Irma ni kimbunga cha kiwango cha tano. Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi cha kimbunga na upepo wake una kasi ya kilomita 280 kwa saa. Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES Image caption Mafuriko huko St Martin Takiban watu milioni 1.2 wameathiriwa na kimbunga Irma na idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa haraka hadi watu milioni 26. Kuna wasi wasi kuwa ugonjwa unaweza kusambaa kwa haraka maeneo ambapo maji ya kunyw...