Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Mfungaji wa goli la kwanza la United Romelo Lukaku akishangilia goli na Juan Mata Michezo nane ya kwanza ya hatua ya mwisho ya makundi ya klabu bingwa barani ulaya imechezwa usiku huu na jumla ya timu kumi na mbili tayari zimefuzu kwa hatua ya kumi na sita bora. Katika kundi A Manchester United, wameibuka vinara wa kundi hilo kwa kuwa na alama 15,baada ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya CSKA Moscow, nao Fc Basel wamesonga mbele kwa kwa kuwa na alama 12 baada ya ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Benfica. Katika kundi B Bayern Munich wamewachapa Paris Saint Germain, kwa kichapo cha goli 3-1 na Celtic wakafungwa 1-0 na Anderlecht hiyo Psg na Bayern ndio wanafuzu kwa hatua inayofuata huku Celtic, wakishiriki michuano ya Europa ligi. Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGE Image caption Mfungaji wa magoli mawili ya Bayern Munich Corentin Tolisso Atletico Madridi wameshindwa kusonga mbele baada ya kukubali sare ya goli 1-1 na Chelsea ugeni...