Posts

Showing posts from August 16, 2017

Watu 600 watoweka kufuatia maporomoko Sierra Leone

Image
Haki miliki ya picha Image caption Shughuli ya uokoaji inaendelea katika mlima baada ya maporomoko kusoma nyumba nchini Sierra Leone Takriban watu 600 wametoweka kufuatia maporomoko ya matope na mafuriko yaliofanya uharibifu mkubwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Freetown nchini Sierra Leone kulingana na msemamji wa rais. Rais Ernest Bai Koroma awali aliomba usaidizi wa dharura akisema jamii nzima ilikuwa imeangamia. Takriban watu 400 wamethibitishwa kufariki baada ya maporomoko ya matope katika eneo la Regent na mafuriko katika maeneo mengine mjini Freertown siku ya Jumatatu. Shjrika la msalaba mwekundu limeonya kuwa hakuna muda wa kutosha kuweza kuwaokoa manusura.Mazishi ya pamoja ya waathiriwa yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano ili kupunguza idadu ya wafu katika chumba cha kuhifadhia maiti. Msemaji wa rais Abdulai Baraytay aliambia BBC kwamba miili ilikuwa ikitolewa katika matope hayoi na vifusi. Jamii nzima inaomboleza. ''Wapendwa wengine w...

RAFIKI SDO NA SAVE THE CHILDREN WAZINDUA MRADI WA ULINZI WA MTOTO,HAKI ZA MTOTO NA UTAWALA

Image
Shirika la Rafiki Social Development Organization – SDO la mkoani Shinyanga leo Jumanne Agosti 15,2017 limezindua Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili katika kata 30 kwenye halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Shinyanga Vijijini na Kahama Mji. Uzinduzi wa mradi huo umefanyika katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.  Akizungumza wakati wa kuzindua mradi huo,Matiro alilitaka shirika hil0 kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa jadi la sungusungu,serikali,viongozi wa dini,kimila na wananchi. “Niwapongeze sana Rafiki SDO kwa kupata mradi huu muhimu kwa ajili ya ulinzi wa watoto,sote tunatambua kuwa vitendo vya ukatili wa watoto vimekithiri katika jamii,serikali pekee haiwezi kumaliza vitendo hivi,lazima tushirikiane ili watoto wetu wawe salama”,alisema Matiro.  “Natamani kusikia mashirika yanajitokeza kuanzisha m...

Wanafunzi wa fani za afya na Sayansi Kupewa Asilimia 40 ya Mkopo Wote Elimu ya Juu (HESLB) 2017/2018

Image
Zaidi  ya wanafunzi 30,000 wa vyuo vya elimu ya juu nchini kwa mwaka mpya wa masomo 2017/18, watanufaika na Sh bilioni 427 kutoka Bodi Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), huku wanufaika hao wakiwekwa kwenye mikondo mitatu. Jana Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul –Razaq Badru alisema kwa mwaka huu wanufaika wasiopungua 30,000 watapata mikopo ya elimu kulingana na fani walizochagua kusoma. Akifafanua idadi na kiwango cha mkopo kitakachotolewa kwa kila mkondo kulingana na fani watakazosoma, Badru alisema bodi imepanga mikondo mitatu ya mikopo.  Mkondo wa kwanza unawahusu wanafunzi wa fani za afya, sayansi ya elimu na hesabu, ambapo kundi hilo litapata asilimia 40 ya mkopo huo ambao ni sawa na Sh bilioni 170.8. Badru alisema kundi hilo ndilo litapata mkopo mkubwa kuliko makundi mengine kutokana na fani hizo kuwa adimu na zina mahitaji makubwa ya soko nchini hasa kwa kuwapata wataalamu watakaosaidia taifa kwenye sekta za afya, sayansi na elimu. Mkondo wa pili u...

Rais Dk Shein aendelea na ziara Mkoa wa Kusini Unguja

Image
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili katika Ofisi ya MKuu wa Mkoa wa Kusini Unguja leo akiwa katika mwendelezo wa ziara zake katika Mkoa huo na kuanzia Wilaya ya Kati Unguja,[Picha na Ikulu.] 15/08/2017. Baadhi ya Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi   Dk.Ali Mohamed Shein (kulia pichani ) alipokuwa akitoa maelekezo baada ya kupokea Taarifa za Utekelezaji Serikali ya Mkoa wa Kusini Unguja na Chama cha Mapinduzi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tunguu katika ziara zake ndfani ya Mkoa huo,[Picha na Ikulu.] 15/08/2017.  Baadhi ya Viongozi mbali mbali waliojumuika katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi   Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo Pichani) wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Nd,Idrissa Kitwana Mustafa  alipokuwa akitoa taarifa ya Utekelezaji ya Mkoa ...