Posts

Showing posts from August 21, 2017

Wanaume 4 washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini

Image
Image caption Wanaume 4 washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini Wanaume wanne wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu. Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu. Kisha polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilipatikana. Wanaume wanne, wawili kati yao madaktari wa kitamaduni walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua. Walifikishwa katika mahakama ya Estcourt kilomita 175 kaskazini magharibi mwa mji wa Durban. Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa kuna uwezekano kuwa wanaume hao wanne walio na umri wa kati ya miaka 22 na 32 ni sehemu ya genge kubwa. Uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa zao wametowewa kujitokeza. Wachunguzi wa visa vya uh...

Wataalumu waonya kuhusu kuundwa roboti zinazoweza kuua

Image
Haki miliki ya picha Image caption Wataalamu hao 116 wametaka kuwekwa marufuku ya kutumia teknolojia hiyo kuunda roboti inayoweza kutumiwa kama silaha. Zaidi ya wataalamu 100 wa teknolojia ya roboti wameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua ili kuzuia kundwa wa roboti zinazoweza kuua. Kwenye barua kwa Umoaj wa Mataifa, wataalamu wa masuala ya teknolojia akiwemo tajiri Elon Musk, wameonya kuwa hatua hiyo itasababisha kuwepo kwa vita vitakavyohusisha roboti. Wataalamu hao 116 wametaka kuwekwa marufuku ya kutumia teknolojia hiyo kuunda roboti inayoweza kutumiwa kama silaha. "Wakati zitaundwa, zitawezesha vita kupiganwa kwa kiwango kingine cha juu na kwa haraka zaidi kuliko vile binadamu hufanya." barua hiyo ilisema. "Hizi zitakuwa silaha za ugaidi, silaha ambazo magaidi watatumia dhidi wa watu wasio na hatia, na silaha ambazo zitadukuliwa kuhudumu kwa njia ambayo sio nzuri." iliongeza Mwaka 2015 zaidi ya wataalamu 1,000 na watafiti waliandika barua w...

Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi ya pamoja ya jeshi

Image
Haki miliki ya picha Image caption Korea Kaskazini tayari imelaani mazoezi hayo ikisema kuwa hatua hiyo ni sawa na kumwaga mafuta kwenye moto. Marekani na Korea Kusini wanafanya mazoezi ya kila mwaka ya jeshi, ambayo mara nyingi huighadhabisha Korea Kaskazini licha ya wito wa kutaka mazoezi hayo yasifanyike. Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilionekana kulegeza kamba baada ya kutisha kuwa itarusha makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam, lakini tena ikasema kuwa itafuatilia mienendo ya Marekani. Korea Kaskazini tayari imelaani mazoezi hayo ikisema kuwa hatua hiyo ni sawa na kumwaga mafuta kwenye moto. Haki miliki ya picha Image caption Mazoezi hayo hujumuisha ya ardhini , baharini na angani China na Urusi mwezi Julai zilipendekeza kusitishwa mazoezi ya kijeshi ili nayo Korea Kaskazini iache kuyafanyia majaribio makombora. Marekani inasema kuwa mazoezi hayo yatawahusisha wanajeshi 17,500 wa Marekani na yatadumu kwa kipindi cha siku kumi. 'Kifaa' cha Korea K...

Manowari ya Marekani yagongana na meli ya mafuta pwani mwa Singapore

Image
Haki miliki ya picha Image caption Manowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini Wanajeshi 10 hawajulikani waliko na wengine watano wamejeruhiwa baada ya manowari ya jeshi la Marekani kugongana na meli ya kubeba mafuta pwani mwa Singapore, kwa mujibu wa jeshi la wanamaji la Marekani. Manowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini wakati iligongana na meli iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Liberia. Shughuli kubwa ya kuwatafuta na kuwaokoa wanajeshi inaendelea Ndicho kisa cha pili kikubwa kinachoikumba meli ya jeshi la wanamaji wa Marekani miezi ya hivi karibuni. Ripoti zinasema kuwa manowari hiyo ilikumbwa na uharibifu upande wake mmoja, lakini jeshi la Marekani lilsema kwa inaelea peke yake kwenda bandari ya Singapore. Image caption Manowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini Helikopta za jeshi la Marekani na jeshi la Singap...