Rais wa zamani wa Georgia Mikheil Saakashvili aingia Ukrain kwa nguvu
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Rais wa zamani wa Georgia Mikheil Saakashvili (katikati)aingia Ukrain kwa nguvu Mikheil Saakashvili ambaye ni rais wa zamani wa Georgia na pia gavana wa zamani wa jimbo nchini Ukrain amevuka na kuingia nchini Ukrain aisaidiwa na mamia ya wafuasi wake. Bwana Saakashvili alisema kuwa alisukumwa bila kutarajia kwenye mpaka na umati wa watu waliokuwa wamekasirika kuwa mpaka ulikuwa umefungwa. "Walitusukuma na kutebeba hadi nchini Ukarain," alesema Saakashvili. Maafisa nchini Ukrain wanasema kuwa aliiangia nchini humo kinyume na sheria na walinzi 15 na mpaka walijeruhiwa. Kulikuwa na mivurutano kwenye mpaka kati ya wafuasi wa bwana Saakashvili na maafisa wa mpaka. Haki miliki ya picha AFP Image caption Mikheil Saakashvili na waziri mkuu wa zamani Yulia Tymoshenko Bwana Saakashvili ambaye awali alikuwa ni raia wa Georgia na kisha raia wa Ukrain kwa sasa hana uraia wa nchi yoyote baada ya uraia wake wa Ukrain kufutwa na m...