Posts

Showing posts from July, 2017

MWENYEKITI CHARLES MAKOGA : SHERIA MPYA KUTUMIKA KUKUZA MAPATO YA MJI WA MAFINGA

Image
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo. Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Mji wa Mafinga wakiwa katika baraza pamoja na wataalamu mbalimbali wa halmashauri hiyo. Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoni Iringa inatarajia kukuza mapato katika mwaka Mpya wa 2017/2018 kutokana na kuanza kuzitumia sheria mpya za ukusanyaji mapato pamoja na kuvijua vyanzo vingine vya mapato ambavyo ndio vitasababisha kukuza uchumi wa halmashauri hiyo. Akizungumza wakati wa baraza la madiwani Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga alisema kuwa sheria mpya walizoletewa toka mwezi wa tano zinawapa nafasi ya kuanza kuzitumia wakati wa kukusanya mapato katika maeneo ambayo walikuwa hawakusanyi. "Tulikuwa hatukusanyi mapato katika maeneo ya stand,sehemu za maegesho ya magari,sokoni na maeneo mengine kwa kuwa sheria zilikuwa bado si rafiki kwetu kwenda kukusanya mapato ila kwa mwaka una...

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yasema Bado Inamtambua Maalim Seif Kama Katibu Mkuu wa CUF

Image
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekishauri Chama cha Wananchi (CUF) kumaliza mgogoro unaoendelea ndani ya Chama hicho kwani unaweza kusababisha kupoteza nafasi za Udiwani katika Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika wakato wowote kuanzia sasa. Tahadhari hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani katika mahojiano maalum Ofisini kwake kuhusu tuhuma  mbalimbali zilizoelekezwa Tume hiyo ikiwemo suala la Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum kupitia CUF. Bw. Kailima amesema mvutano unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) hauna tija, hivyo ameshauri pande mbili zinazovutana kukutana na kumaliza tofauti zao kwani hali hiyo itawanyima nafasi ya kutoa wagombea kwenye uchaguzi huo mdogo. “Mimi niwashauri, CUF wana mgogoro wao wamalize mgogoro wao. Ni vizuri wakutane wamalize mgogoro wao kwani hii inaweza kuwaletea matatizo wagombea wakati wa Uchaguzi.’  alisesema Kailima na kusisitiza kuwa mgogoro ndani ya chama hicho hauna tija n...

TRA YAFUNGA MADUKA YA WASIOTUMIA MASHINE ZA EFD MKOANI IRINGA.

Image
    Hatua hiyo imekuja baada ya maofisa wa TRA kufanya ukaguzi wa kushitukiza katika maeneo mbalimbali ya mji wa Iringa na kubaini uwepo wa wafanyabiashara wanaodaiwa kutokuwa na mashine za kutolea risiti za EFD. Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa, Ndg Lampson Tulianje amesema wafanyabishara hao wamekaidi agizo la Serikali la kutakiwa kuwa na mashine kwa zaidi ya miezi mitatu. “Tumewapa maagizo, tumewahamasisha kwa zaidi ya miezi mitatu lakini bado wamekaidi agizo letu, uamuzi tuliochukua ni kufunga duka na mara atakaponunua tunamfungulia duka lake,”amesema Tulianje . Tulinje amefafanuaa kuwa lengo la kufikia hatua hiyo ni kuhimiza wafanyabiashara hao kulipa kodi stahiki kwa kutumia mashine hizo ambazo zina uwezo wa kuweka kumbukumbu vizuri za mauzo ya bidhaa zao. Pia Tulinje ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kuacha kushindana na Serikali badala yake kuhakikisha wananunua mashine hizo na kuzitumia kwa kuwa hata gharama wanazotumia zinarudishwa na TRA wakati wa kuk...

Mazoezi ya Kijeshi ya Kihistoria Kufanyika Nchini......Yanahusisha Majeshi ya Nchi 7 za SADC

Image
Vikosi maalumu vya majeshi ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) vimepiga kambi kwenye eneo la mapango ya Amboni, Tanga kwa ajili ya mazoez ya kijeshi. Katika mapango hayo, mwaka jana yalitokea mauaji yaliyofanywa na watu wasiojulikana na kuzua hofu kwa wakazi wa eneo hilo ambao mwishowe walihamishwa na Serikali. Akizungumza na waandishi wa habari   jana, Mkuu wa mpango huo, Meja Jenerali Harrison Msebo, alisema vikosi hivyo vitakuwa vikifanya mazoezi katika eneo hilo kama sehemu ya kupambana na ugaidi na uharamia baharini. Kwa mujibu wa Meja Jenerali Msebo, mazoezi hayo yajulikanayo kwa jina la EX Matumbawe, yanatarajia kuanza Agosti 2 hadi Septemba mosi mwaka huu. “Mazoezi hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza  Tanzania baada ya vikosi vya majeshi ya nchi washirika kuanza kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya kujihami dhidi ya matukio mbalimbali ya uhalifu tangu mwaka 2015. “Pamoja na mambo mengine, lengo l...

UNCDF YAWEZESHA UFUGAJI SAMAKI KIBIASHARA BWAWA LA KALEMAWE

Image
SERIKALI ya Tanzania, imeshukuru Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) kwa kuwezesha watanzania kupambana na umaskini kupitia miradi wanayoidhamini au kuitafutia fedha. Kwa miongo miwili UNCDF imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) katika mpango wa kupeleka madaraka kwa umma na shughuli za maendeleo ya kiuchumi. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Aisha Amour kwenye ufunguzi wa kongamano la siku 2 la Wadau wa Ufugaji Samaki Kibiashara Bwawa la Kalemawe lililoko wilaya ya Same mwishoni mwa wiki.  “Tunafurahishwa kwa namna ya pekee na UNCDF kwa jitihada zake zinazoendeshwa kupitia katika Mpango wa Ufadhili Miradi ya kiuchumi (LFI),” alisema Iyombe na kuongeza: “Tunapokutana hapa tunapewa fursa na kufunuliwa uzoefu wa ushiriki wa UNCDF k...

MTANDAO MPYA WA VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII WASAJILIWA NCHINI

Image
Mtandao mpya unaoundwa na Radio na vyombo vya habari vya kijamii Tanzania chini ya shirika la vyombo vya habari vya maudhui ya kijamii uliosajiliwa kwa jina la TANZANIA DEVELOPMENT INFORMATION ORGANIZATION-TADIO umeanzishwa rasmi baada ya kuvunjika kwa mtandao wa zamani wa COMNETA. Tukio hilo limetokea Julai 28, 2017 katika mkutano mkuu wa kwanza ambao pamoja na mambo mengine ulichagua safu mpya ya viongozi wa mtandao huo. Shirika la mtandao wa vyombo vya habari jamii Tanzania uliokuwa na jina la COMMUNITY MEDIA NETWORK OF TANZANIA – COMNETA, limevunjika rasmi mwezi machi mwaka huu. Katika mkutano huo kuwa kuundwa kwa shirika hilo jipya kunalenga kuhakikisha kunakuwa na mtandao makini wa Radio na vyombo vingine vilivyojikita katika kuibua kwa kuandika na kutangaza masuala ya kijamii kwa ajili ya maendeleo.  Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe wakati wa mkutano huo. Akihutubia katika mkutano huu kaimu mkuu wa ofisi ya UNESCO Tanzania, amb...