![]() |
HIKI NDICHO KIFAA WANACHOTUMIA KUWAPA JOTO WATOTO WALIOZALIWA CHINI YA UZITO(NJITI) |
GOR MAHIA MABINGWA WA SPORTPESA SUPER CUP 2017, SASA KUKIPIGA NA EVERTON JULAI 13
Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, (wa pili kulia) akikabidhi Kombe la SportPesa Super Cup kwa Nahodha wa Gor Mahia, Shakava Haron, baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AFC Leopards katika mchezo wa fainali uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar Timu ya Gor Mahia ya Kenya imetwaa ubingwa wa kwanza wa mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kuwasambaratisha wapinzani wao, AFC Leopards kwa mabao 3-0 kwenye uwanja wa Uhuru. Uliozikutanisha timu zote za Kenya uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Gor Mahia imepata nafasi ya kupambana na timu maarufu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Everton FC Julai 13 kwenye uwanja wa Taifa jijini. Mshambuliaji wa Gor Mahia na mfungaji wa bao la kwanza kati ya matatu, Muguna Kenneth, akimtoka beki wa AFC Leopards, Abdallah Salim, wakati wa mchezo wa Fainali...
Comments
Post a Comment