January makamba achukua fomu ya ugombea urahisi.
Mbunge wa jimbo la Bumbuli, mjumbe wa NEC na Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba baada ya kutangaza nia jana juni 10, amechukua fomu katika Ofisi Kuu za Chama Cha Mapinduzi mjni Dodoma ya kuomba kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu Makmba alisema kwamba ataendelea na safari yake nchi nzima kutafuta wadhamini ambao ni wanachama wa CCM ikiwa ni sehemu ya hitaji la chama kuwa na wadhamini 450.
Hata hivyo aliwashukuru wananchi kwa kuungana naye kutoka katika kila kona ya nchi na nje ya nchi huku akisisitiza kuwa ni zama mpya, za kizazi kipya kuamua na kujenga kesho ya nchi yetu
Comments
Post a Comment