VIDONDA VYA TUMBO.

 
VIDONDA VYA TUMBO,DALILI NA MATIBABU YAKE
Imekuwa ni changamoto sana kwa watu wanaosumbuliwa na vidonda vya tumbo hii ni kwa sabubu zifuatazo
1.       Jamii haijatambua kuwa vidonda vya tumbo husababishwa na mienendo ya maisha yetu. Hivyo tiba yake kuu ni kubadili maisha tunayoishi nayo,kuanza lishe tunayopata,jamii tunayo ishi nayo, na kuepuka vinywaji vinavyo hatarisha afya ya ukuta wa mfuko wa chakula.
2.       Dawa kama omeprazole na zingine nyingi ambazo kwa pamoja tunaziita PROTON PUMP INHIBITORS zinapunguza utoaji wa asiodi ambayo ikitolewa kwa wingi inaenda kuharibu kuta za mfuko wa chakula. Hivyo zinazuia tu tindikali bila kushugulika na chanzo cha kuongezeka kwa hiyo tindikali. Hivyo bila kuondoa chanzo kinachosababisha kuongezeka kwa tindikali hiyo ya HCL hata siku moja huwezi kupona ndio mana siku hizi kuna dawa za kutuliza kama mmoja wapo wa wagonjwa nilikutana nae anasema hivyo. Inaweza kuwa leo hii na wewe umebahatika kusoma makala hii hivyo napenda nikuambie kuwa tiba ya vidonda vya tumbo ni wewe mwenyewe na tiba yake unayo hapo nyumbani tatizo ni kwamba tumeshaga kalili tu kwamba tiba lazima uikute madukani inauzwa.. vidonda vya tumbo vinatibika pata elimu ya lishe na badili tabia yako hakika utapona.

3.       Hizi dwa za vidonda vya tumbo zinatakiwa zitumike pale panapohitajika siyo maisha yako yote. Kwani hizi dawa mara nyingi huja na maudhi mbalimbali kwani ni dawa ambazo zimetengenezwa kwa chemikali. Dawa pekee ambazo ni sahihi kwa matumizi na zina madhara kidogo ni zile ambazo ni asili. Changamoto kubwa kwa hapa Tanzania ni kuwa huduma hii bado haijapata wataaalamu waliobobea wakaanza kutoa bidhaa bora na zenye kufanyiwa utafiti wa kutosha na zenye kiwango cha kimataifa.
4.       Tunapenda kula vyakula vyenye sukari nyingi,vyakusindika,viwandani na vyenye viungo vingi hivi vyote ndio visababishi vyakutolewa kwa tindikali ya HCL mwilini ambayo ikizidi inaharibu kuta za tumbo. Hivyo ni wakati sasa wa kurudi katika vyakula ambavyo bibi na babu zetu walivyo kula. Ni ukweli usiopingika kuwa vyakula vya super markert ni vya bei ya chini kuliko vyakula vya matunda, na mboga mboga. Je umeshaga jiuliza kwa nini hivyo vyakula vinauzwa kwa bei ndongo!!!  Fanya uchunguzi huu juice ya zabibu lita moja ukiitengeneza wewe ya asili itagharimu shilingi ngapi!! Na je lita moja ya zabibu juisi kiwandani ni shilingi ngapi!! Ifike sehemu tubadirike kwani tiba ipo nyumbani na vyakula tunavyokula ndivyo vinaangamiza jamii. Nalijua hilo mtanzania anapokuwa ana afya njema ni mjuaji sana kuhusu afaya yake laikini waswahili walisema mganmga hajigangi.
VIDONDA VYA TUMBO NINI??
>Ni kuharibika kwa ukuta wa tumbo la chakula na sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba
Kuna aina kuu mbili za vidonda vya tumbo
1.       Gastric ulcers-hivi hutokea kwenye mfuko wa tumbo la chakula
2.       Duodenal ulcers-hivi hutokea sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba
VISABABISHI VIKUU VYA VIDONDA VYA TUMBO
1.       KUONGEZEKA KWA TINDIKALI YA HCL KWENYE TUMBO LA CHAKULA
>imekuwa ni changamoto kubwa sana kwani moja ya visababishi hivi kila siku tunakumbana navyo ndiyo maana kwa nchi kama Tanzania kutibu vidonda vya tumbo ni changamoto kubwa.
VIFUATAVYO HUONGEZA TINDIKALI YA HCL
A.      MAWAZO
Watu wengi tunasumbuliwa na changamoto hii ya kushambuliwa na msongo wa mawazo kila siku hii inatokana na kutojua namna ya kushughulika na msongo wa mawazo. Jifunze namna ya kuepuka msongo wa mawazo utaona mabadiliko yakitokea .
B.      Madawa mbalimbali
Ø  Imekuwa ni desturi sisi kutumia dawa kama diclofenac,aspirin na zingine nyingi kama makande. Dawa hizi huzuia utengenezaji wa uteute unaolinda ukuta wa tumbo na hivyo kushambulia kwa kasi kwa ukuta wa tumbo. Pia dawa hizi huzia utengenezwaji wa ukuta wa tumbo na hatimaye ukuta kudhoofika na kuanza kushambuliwa na tindikali. Pia dawa hizi zinaua bacteria wanao stahili kukaa tumboni yani normal flora na kufanya wadudu nyemelezi kama helicobacter pylori kushambulia ukuta wa tumbo. Kuwepo kwa walinzi hawa huyo mdudu anaye sababisha vidonda vya tumbo hata siku moja hawezi kushambuliwa. Hivyo kuwalinda bakiteria hawa ni kuhakikisha tunawalisha chakula kinachowafanya waendelee kustawi na kukulinda. Jiulize ni chakula gani kinafaa?? Jibu ni vyakula vitokanavyo na mimea na matunda hufanya bactria walinzi wetu watulindi kwa umahili mkubwa.
C.      Uvutaji wa sikara na kunywa pome sana
D.      Vyakula vibaya tunavyokuwa kila siku
DALILI ZA VIDONDA VAYA TUMBO
1.       Tumbo kuwaka moto sehemu ya juu kulia na endapo maumivu yakizidi husambaa hadi mgongoni.
2.       Njaa hasa wakati wa usiku saa kumi na moja asubuhi utasikia tumbo linawaka moto
3.       Tumbo kujaa gesi sana
4.       Kichefu chefu na kuharisha kutokana na kubagua vyakula
5.       Inaweza kupelekea kutapika damu,kuishiwa damu na hatimaye kifo kama mgonjwa asipo wahishwa hospitali
6.       Kutoa choocheusi ni kiashiria damu inavia sehemu ya juu ya tumbo.
UKIONA DALILI KAMA HIZI TAFADHARI MUONE DAKTARI
VYAKULA VYA KUEPUKA KABISA
1.       Vyakula vyenye viungo vingi.
2.       Vyakula au kinywaji chenye caffeine hivyo angalia label kama wewe ni muhanga wa vyakula vya viwandani na hutaki kuacha.
3.       Pombe ya aina yoyote
4.       Vyakula vyote vya ngano nyeupe kama mikate nk kwani zina glutten
5.       Vyakula vya sukari nyinngi pia vinywaji vya sukari nyingi. Hii ni kwa sababu ulapo au unywapo sukari nyingi inalisha bakiteria wabaya na hatimaye hao bacteria wazuri kufa na hawa wabaya kuanza kushambulia kuta za tumbo la chakula. Hivyo sukari huenda kulisha bacteria wabaya.
HIVI NI VYAKULA VIKUU VYA KULA KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
MATOKEO NI NDANI YA MUDA MFUPI TU.
1.       KULA CHAKULA KIDOGO KIDOGO
Ø  Hii ina maaana unatakiwa kuepuka kitendo cha kula chakula kingi kwa mara moja. Tenga chakula chako na kigawanye ule mara nyingi hii ni kwa sababu unapokula chakula kingi kwa wakati mmoja kunasababisha mmengenyo wa chakula utaenda polepole na hivyo kuzidi kuathiri zaidi ukuta wa tumbo. Pia tunashauri ule mara kwa mara ili kufanaya chakula cahako kifanyiwe kazi ipasavyo bila mrundikano na pia kupunguza maumivu ya tumbo.
2.       KULA VYAKULA VYA NYUZINYUZI AU FIBER
Ninapo ongelea fiber nina maaanisha kutoka kwenye mboga mboga na matunda pia nafaka kidogo. Hakikisha kila siku unatapata angalau 30gm za fiber itakusaidia na kukubadilisha maisha kabisa. Kwani utafiti unaonesha kuwa fiber inaongeza wingi wa kichocheo cha LEPTIN ambacho hukusaidia wewe ule kwa kiasi pia zinakata ulaji mwingi wa sukari pia inakufanya ukae muda mrefu tumbo likiwa limeshiba. Hivyo hapo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja kwani umezuia aside,umeakata ulaji wa sukari na hakuna maumivu tena ya njaa. Swali la kujiuliza ni vyakula gani vina fiber nyingi?? Vyakula vipo vingi lakini jitahidi sana kutumia juice na mboga za majani ulizo zipika kwa mvuke pekee kwani zina fiber nyingi sana ppia kuna matunda yani wengi mkubwa wa fiber karibuni tujifunze mengi.
3.       JUICE YA KABEJI
Imekuwa ni furaha iliyoje nataja mboga ambayo kila siku tunaona ni mboga ambayo haina manufaa kwetu. Kwani utafiti unaonesha kuwa kabeji ina alkali ambayo hupunguza makali ya tindikali pia ina wingi wa vitamin C na viambata vingine mahususi ambavyo hufanya wale bacteria wazuri wale vizuri na watulinde na magonjwa nyemelezi kama huyo h. pylori. Pia ina VITAMINI K AMBAYO INA KAZI KUBWA SANA YA KUPONYESHA KABISA KUTA ZA MFUKO WA CHAKULA.
MATUMIZI
Andaa kabeji yako na uoshe vizuri hakikisha una APPLE MBILI NA CARROTI HATA MBILI katakata weka kwenye Brenda kasha saga kwa muda wa dakika 5-8 tumia juice hii mara tatu kwa siku asubuhi mchana na jioni kabla ya kula chochote kaa nusu saa kula chakula.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi