Iringaland.blogspot.com ni blog inayohusu vivutio na matukio mbalimbali yanayotokea duniani na Masuala ya Afya kwa ujumla na pia kuna vivutio vingi zikiwepo sehemu za historia mbuga za wanyama misitu mikubwa,sehemu za historia nyingi na mengine mengi yanapatikana kwenye blog hii.wote mnakaribishwa kutangaza kupitia kurasa yetu ya iringaland.blogspot.com na Email:lufumbe@gmail.com Instagram @lufumbe
Gereza la Guantanamo lakaribia kufungwa
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Gereza la Guantanamo lakaribia kufungwa
gereza la Guantanamo linamilikiwa na Marekani
Ikulu
ya White house imesema kuwa mipango ya kulifunga gereza la Guantanamo
Bay nchini Cuba imefikia awamu za mwisho. Rais Barack Obama anasemekana
kupatia kipa umbele suala la gereza hilo tangu aingie madarakani mwaka
wa 2009 lakini limekumbwa na vizuizi kadhaa.
gereza lililo n aulinzi mkali la Guantanamo
Gereza hilo la Guantanamo,
ambalo limepewa jina la umaarufu kuwa Gitmo - limekuwa likitumiwa na
Marekani kuwazuilia wapiganaji kutoka vita vya Iraq na vya Afghanistan
bila kufunguliwa mashtaka yoyote. Rais Obama alitoa agizo la kirais
kufungwa kwa kituo hicho mara moja katika siku yake ya kwanza. Lakini
baraza la Congress lilikataa kuwahamisha wafungwa wa huko kuwaleta
nchini Marekani kutokana na hofu za kiusalama. gereza la Guantanamo
Baadhi ya wadadisi wanaamini
kuwa Marekani ilifungua gereza hilo nje ya ardhi ya Marekani ili
wanajeshi wake wapate fursa ya kutumia mbinu zilizopigwa marufuku katika
ardhi yao za kuwahoji wafungwa.
Gereza hilo pia limekumbwa kwa
miaka mingi na madai ya ukiukajji wa haki za binadamu, ambapo njia
zilizotumika kuwahoji wafungwa zimekashifiwa kuwa ukiukaji mkubwa wa
haki za binadamu. Aidha wafungwa wengi wamedai kuteswa, kupigwa na hata
kulazimishwa kukiri baadhi ya mashtaka. wafungwa katika gereza la Guantanamo wamedai kuteswa
Wafungwa kadhaa maejaribu
kujitoa uhai kutokana na mateso wanayodai kupata huko. Wengine
wamechukua hatua kama kususia kula kwa wiki kadhaa kama njia ya
kulalamika hali duni ya kibinadamu katika gereza hilo. wafungwa kadhaa wamereshwa makwao
Wengi tayari wamerejeshwa nchini mwao japo kunao baadhi ambao wanaaminiwa kuwa hatari zaidi na hivyo hawaja achiliwa.
Msemaji
mmoja wa ikulu ya white house ameambia waandishi kuwa mipango ya
kuwasafirisha wafungwa hao kwa njia salama imefikia awamu za mwisho na
itawasilishwa kwa baraza la Congress, lakini hakutoa maelezo zaidi
Ili iitwe sabuni inatakiwa -Ngumu kuiisha -Yenye povu jingi -Nyeupe VIAMBATA VYA kutengenezea sabuni Mafuta-mawese,mise,wanyana Maji Caustic soda(costiki soda) VIFAA VYA KUTENGENEZEA Ndoo za plastiki lita 20 nne Diaba 1 Mti wa kukorogea Mashine ya kukorogea Box la kugandishia Mhuri wa biashara Mzani wa saa Vibao vya kukatia VIFAA VYA USALAMA Mask Groves Gum boots Goggles (miwani) Overall Ndoo ya maji au mchanga FORMULA mafuta lt1+caustic soda grm135+maji mls350+sodium siligate prm100. KUCHANGANYA pima maji ktk ndoo ya plastic kisa weka caustic soda ktk maji weka kidogokidogo huku ukikoroga mpaka itakapo yeyuka.mchanganyiko huu unaweza kuchemka na kutoa mosh usiogope. acha ipoe kuanzia masaa 8 nazaidi. KUCHANGANYA NA MAFUTA yeyusha mafuta kwa kuyapasha joto kidogo ambapo unaweza kuyashika, tia sangi na mimina kidogo2 kuchanganya michanganyiko huku ukikoroga. mimina kwenye box la kugandishia acha igande tayari kwa kukata.Pia weka sodium siligate
Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi Hatua ya kwanza Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki. Hatua ya pili Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke. Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa. Hatua ya tatu Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi. Njia ya pili Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo. Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla sabuni haijawa ngumu mwaga sabuni ndani ya kasha la mba...
Image caption Mshambuliaji mpya wa klabu ya Arsenal Alexandre Lacazette Mshambuliaji mpya wa klabu ya Arsenal Alexandre Lacazette jana jumatatu usiku alifanikiwa kuifungia mabao 2 - 0 dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa Ligi kuu ya England , kwa bao la dakika ya 20 kipindi cha kwanza na bao lingine la dakika ya 67 kipindi cha alilofunga kwa njia ya penati. Alexandre Lacazzete mpaka sasa amevunja rekodi ya Brian Marwood iliyowekwa mwaka 1988 ya kufunga katika michezo mitatu ya mwanzo ya ligi ya Epl. Kwa matokeo hayo yanawafanya Arsenal kubaki katika nafasi ya saba ya msimamo wa ligi kuu Uingereza wakiwa na alama zao 10 huku Manchester City wakiwa kileleni.
Comments
Post a Comment